Tanzania yapokea msaada wa Sh26 bilioni

Muktasari:

  • Mashirika matano yasiyokuwa ya kiserikali yamepewa msaada wa zaidi ya Sh26 bilioni kwa ajili ya utekelezaji miradi yao ikiwemo uendelezaji misitu na njia Jumuishi ya Mabadiliko ya Mnyororo wa Thamani wa nishati ya kuni.

Dar es Salaam. Mashirika matano yasiyokuwa ya kiserikali yamepewa msaada wa zaidi ya Sh26 bilioni kwa ajili ya utekelezaji miradi yao ikiwemo uendelezaji misitu na njia Jumuishi ya Mabadiliko ya Mnyororo wa Thamani wa nishati ya kuni.

Miradi hiyo pia itaimarisha juhudi za nchi katika kukabiliana na matumizi ya kuni, sababu kubwa ya ukataji miti na uharibifu wa misitu nchini, kuimarisha mifumo ya kisheria na kitaasisi ya usimamizi endelevu wa misitu, kupunguza kiasi cha biomass kinachotumika, na hivyo kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa gesi joto.

Fedha hizo zilizotolewa na Umoja wa Ulaya na kupokeleea na Serikali kwa niaba ya Mashirka hayo zinatajwa kwenda kunufaisha wananchi kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Morogo na Pwani.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo mitano, Naibu Katibu Mkuu anayesimakia fedha za nje kutoka Wizara ya Fedha, Amina Khamis Shaban amesema utekelezaji wa miradi hiyo utaleta matokeo chanya katika ajenda ya maendeleo ya Tanzania.

“Pia miradi hii ni ni sehemu ya ajenda pana ya Serikali inayolenga kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kutokana na ukataji miti na uharibifu wa misitu. Miradi hii inalenga kufikia matokeo yafuatayo,” amesema Amina.

Amesema utekelezaji wa miradi hiyo, kutawajengwe uwezo wananchi ikiwa ni pamoja na wazalishaji na watumiaji wa kuni kushiriki katika mazoea endelevu ya usimamizi wa misitu kando ya mnyororo wa thamani ya nishati ya kuni.

Amesema kusainiwa kwa mikatqba hiyo inaonyesha ni kiasi gani Serikali iko tayari kufanya kazi na mashirika yasiyokuwa yabkiserikali.

"Hili linafanyika ili kufikia maendeleo yanayoyegemeea kupitia mipango ya muda mrefu ya nchi. Fedha hizi pia ni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kutafuta mbinu jumuishi kwa ajili ya kutafuta suluhisho la nishati ya kupikia,"

Akifafanua baadhi ya mikataba hiyo, mmojawapo ni utakaogharimu Sh5.26 bilioni zitakwenda kutekeleza mradi wa Uwezeshaji jamii katika usimamizi endelevu wa misitu na nishati mbadala (USEMINI) katika Mkoa wa Morogoro katika wilaya za Mvuha, Kilombero, Malinyi na Ulanga.

Mradi huo utatekelezwa na shirika la Helvetas Swiss Intercooperation (Helvetas) likishirikiana na Mtandao Wa Jamii Wa Usimamizi Wa Misitu Tanzania (Mjumita) na Community Development and Relief Trust (Codert) ndani ya miezi 36.

Mkataba mwingine ni ule unaolenga Kukuza Mnyororo wa Thamani ya Mkaa Endelevu unaotarajiwa kutekelezwa mkoani Pwani katika wilaya za Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Kibiti na Rufiji huku ukigharimu zaidi ya Sh4.01 bilioni.

Mradi huo wa miezi 36 pia utasimamisa na shirika la Shirika la Kuendeleza Nishati Tanzania (TaTEDO) likishirikiana na Taasisi ya jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF)

"Pia kutakuwa na mradi utakaotumia Sh5.26 bilioni unaohusu Suluhu Jumuishi za Misitu na Nishati ya Biomasi kwa Tanzania (IFBEST) utakaotekelezwa Mkoa wa Tanga katika wilaya za Handeni, Kilindi, Mkinga na Pangani,"

Mradi huo utafanyika chini ya shirika la Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) likishirikiana na Mtandao Wa Jamii Wa Usimamizi Wa Misitu Tanzania (MJUMITA).

Miradi mingine itakayotekelezwa ni ule wa kutengeneza njia jumuishi ya mabadiliko ya mnyororo wa thamani wa nishati ya kuni huku mwingine ukilenga kuharakisha upandaji miti kwa ajili ya maendeleo ya kaya mkoani Tanga.

Amina alitumia nafasi hiyo kuwataka wanufaika kutekeleza mikataba kwa kuzingatia vigezo na masharti na kutumia ipasavyo rasilimali watu kutoka maeneo ya miradi ili kuongeza umiliki na uendelevu wa miradi.

Mkuu wa Ushirikiano, Ubalozi wa umoja wa Ulaya nchini, Cedric Merel alisema uchaguzi wa mashirika hayo yasiyokuwa ya ulizingatia uzoefu katika sekta ya misitu na ushirikiano na jumuiya za vijijini, afua juu ya usimamizi endelevu wa misitu ni biashara zao kuu.

“Ni matumaini yetu kwamba NGOs hizi zitatoa matokeo yanayotarajiwa na kuchangia katika kufanya mnyororo wa thamani ya kuni kuwa endelevu zaidi, usawa na manufaa kwa jamii," amesema Merel na kuongeza

"Tutafuata na kufuatilia kazi zao kupitia kamati ya uongozi pamoja na wizara za nishati, maliasili na fedha ili kuhakikisha kuwa fedha hizi zinasimamiwa kwa ufanisi na kwa ufanisi; kwa hivyo tafadhali washirika wapendwa hutumia vizuri fedha hizi.