Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maofisa matatani wakidaiwa kuua mfanyabiashara

Muktasari:

  • Mkazi wa Muriet jijini Arusha, Issa Mbaruku aliuawa Novemba 7, 2023 katika eneo la Lokisale wilayani Monduli baada ya kupigwa risasi ya miguu na kufariki njiani katika harakati za kumpeleka kituo cha afya Lokisale.

Monduli. Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia maofisa wawili wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) kwa tuhuma za kumpiga risasi mfanya biashara wa mkaa jijini Arusha na kumsababishia kifo.

Kijana huyo Issa Mbaruku (27) mkazi wa Muriet jijini Arusha aliuawa Novemba 7, 2023 katika eneo la Lokisale wilayani Monduli baada ya kupigwa risasi ya miguu na kufariki njiani katika harakati za kumpeleka kituo cha afya Lokisale.

Akizungumza na Mwananchi, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP, Salvas Makweli amesema kuwa maofisa hao wanashikiliwa kwa upelelezi na ukikamilika watawafikisha mahakamani

“Kwa sasa siwezi kuwataja majina kutokana na mazingira yenyewe ya tukio, ila bado upelelezi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa kamili hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikisha mahakamani,” amesema.

Mashuhuda wa tukio hilo, wamedai kuwa siku ya tukio majira ya mchana katika eneo la Ndukusi walikutana na maofisa hao wakiwa katika mzozo wa kutaka kumnyan’ganya mmoja wa vijana pikipiki yake iliyokuwa imebeba mkaa ndipo kuuliza tatizo wakajulishwa kuwa anatakiwa kutoa hela ya faini ya kubeba mzigo huo.

“Mimi nikiwa na mzigo wangu napita nikaona maofisa hao wakiwa na pikipiki isiyo na plate namba (namba za usajili), wanamnyang’anya pikipiki yenye mkaa kijana wetu mmoja wakitaka shilingi 50,000 ya faini, jamaa akamwambia mimi nina 12,000 tu hapa lakini uzuri akatokea mwingine akaongeza 3,000 ikawa 15,000 lakini bado wakakataa” amesema Amani Jacob na kuongeza.

“Baada ya punde wakapita wenzetu akiwemo huyu Issa aliyeuawa akaanza kupinga tukio hilo akitaka tukae tuelewane lakini wale maofisa wakakataa maelewano bila hela kujaa ndio mzozo ukatokea hadi kufikia kupiga risasi mbili hewani na mbili za miguu kila mmoja akakimbia na wao wakatoweka,” amesema.

Naye Elisaria Msuya amesema kuwa hilo tukio sio la mara ya kwanza walazimishwa kutoa hela na maofisa hao wa maliasili wanapokutana nao kwa matisho ya kuwapora pikipiki zao na kwenda kuwabambikia kesi za kukutwa na nyamapori.

“Tunaomba Serikali itusaidie maana hii biashara tunalipa ushuru na tunapita katika mageti yote ya pori kihalali maana kila geti tunajulikana na kodi tunalipa lakini tunateseka kila tukikutana na hawa jamaa na kutokana na uoga wetu tunalazika kutoa hela lakini sasa wanazidi kupanda dau kila kukicha na kuua vijana wetu,” amesema.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndukusi, Loi Sironga amesema siku ya tukio alipigiwa simu na mmoja wa wananchi wake akipewa taarifa za tukio hilo na alipofika alikuta vijana wamempeleka mwenzao katika Kituo cha Afya, Lokisale.

“Mimi nilipoambiwa nilikwenda eneo la tukio na kukuta hawapo na kwenda kituo cha Lokisale kupata maelezo ya tukio la hapo hapo nikampigia Ofisa Maliasili wetu na akathibitisha kupata taarifa na anashughulikia lakini ninachosikitika ni kwanini wasababishe tukio na kuacha mwili eneo la tukio na kukimbia hata wasimpe msaada kama kweli walikuwa hawana lengo baya la kuua?” alisema Loi.

Mkuu wa Idara ya Maliasili Wilaya ya Monduli, Adili Mwanga amesema kuwa wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za maofisa wake kusababisha tukio hilo.

Amesema kuwa vijana hao ambao wanalinda eneo la Lokisale, Laalarami, Meserani na Moita, wamepatwa na kadhia hiyo katika eneo la kikazi ambapo wanalifuatilia zaidi kujua chanzo.

“Tukio limetokea mazingira ya kikazi ambapo vurugu hizo huwa zinasababishwa na vijana wa bodaboda kufanya uharibifu wa mazingira upande wa misitu na wanyamapori na kuchukua bidhaa za rasilimali hizo bila utaratibu” alisema na kuongeza

“Mimi nilivyopata taarifa ni kuwa vijana hao walivyoonekana na maofisa wetu walisimamishwa lakini hawakutaka kutii amri bila shuruti na kwa sababu wanatembea katika makundi huwa wanashika mapanga na kuleta taharuki hivyo nadhani katika utaratibu huo wa kuulizana na kutoelewana na kutishana ndio yakatokea haya mauaji,” amesema.