Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tathmini mkataba mpya bandari yaleta matumaini

Muktasari:

  • Tathmini ya ufanisi wa utendaji wa mkataba kati ya kampuni ya DP World na Serikali ya Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa mambo muhimu katika mkataba huo.

Dar es Salaam. Tathmini ya ufanisi wa utendaji wa mkataba kati ya kampuni ya DP World na Serikali ya Tanzania uliosainiwa Oktoba 22, imetajwa kuwa miongoni mwa mambo muhimu yaliyotarajiwa na wananchi.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 25 na Mhariri wa Uchumi wa gazeti la Mwananchi, Ephraim Bahemu alipokuwa akichangia maoni yake katika Mwananchi Space iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) ikiwa na mada ya ‘Mkataba bandari umekidhi matarajio ya wananchi?"

Hafla ya usainishaji wa mkataba wa DP World na Serikali ya Tanzania (HGA) ilifanyika Oktoba 22, 2023 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kushuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine akiwemo Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Bahemu amesema kufanyika kwa tathmini katika mkataba huo kutatoa fursa muhimu kuona kama matarajio ya watu.

"Tayari kulikuwa kumeanza kuwa na minong'ono kuwa uwekezaji ni mdogo ikilinganishwa na ukubwa wa biashara ya inayifanyika bandari ya Dar es Salaam pia Serikali ilikuwa imewekeza hivi karibuni baada ya kukopa fedha kuimarisha bandari.

"Sheria haziruhusu mikataba ya kibiashara kuwekwa wazi, lakini angalau kwa wananchi kupewa dondoo ya baadhi ya mambo muhimu yaliyopo katika mkataba huo nafiriki kwa kiasi fulani ilitibu kiu ya wengi," amesema Bahemu.

Hata hivyo, akichangia katika mjadala huo, Msemaji mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesisitiza kuwa kuwekwa wazi kwa mikataba hiyo hakuruhusiwi kwani ni makubaliano ya kibiashara kati ya pande mbili.

Kwa upande mwingine, Mhariri wa Siasa wa Mwananchi, Peter Elias amesema akivhabgia mjadala huo, matumizi ya sheria za Tanzania katika utekekelezaji wa  mkataba huo ni kitu kilichokata kiu ya wengi, kwani awali katika mkatababwa mamubalianobkati ya Serikali ya Dubai na ya Tanzania ilielezwa kuwa utatuzi wa migogoro utafanyika Afrika Kusini.

"Wito wangu ni kwamba, wananchi wanataka kuona matokeo kwani wamekuwa na matumaini makubwa sana kwenye huu mkataba," amesema.