Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TBS yaanzia mfumo mtandaoni kusajili ubora bidhaa

Ofisa uhakiki ubora Shirika la Viwango nchini(TBS)  Hassan Juma akizungumza na mjini Morogoro juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa kimtandao utakaosaidia kuraisisha usajili wa alama za ubora wa bidha.(Lilian Lucas)

Muktasari:

TBS yaanza kutumia mfumo wa kimtandao kuraisisha usajili wa alama za ubora wa bidhaa

Morogoro. Shirika la  Viwango Tanzania (TBS) limewahimiza wananchi kuanza kutumia mifumo ya kimtandao ili kurahisisha usajili wa alama za ubora wa bidhaa ambao kwa sasa unatumika na kuwafanya kupata huduma kwa haraka za shirika hilo tofauti na ilivyokuwa awali.
Afisa Uhakiki Ubora wa TBS, Hassan Juma alisema hayo wakati akizungumza na Mwandishi wa Mwananchi mjini Morogoro baada ya kumalizika maonyesho ya Wiki ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Juma alisema katika kuhakikisha bidhaa zinaendelea kuwa na ubora na kuthibitishwa limeamua kuanza kutumia mfumo ya kimtandao kwa Watanzania hususani wale wanaotoka maeneo ya mbali kuacha kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.

Aidha, alisema shirika hilo limeendelea kushughulika na kuandaa, kusimamizi wa viwango mbalimbali la bidhaa Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya alama ya ubora katika bidhaa zinazozalishwa nchini huku likihakikisha kwamba bidhaa zinazoingi katika soko ya Tanzania kutoka nje zimedhibitishwa ubora wake na kukidhi matwakwa ya viwango vya ndani na vile vya kimataifa kwa bidhaa ambazo bado hazina viwango vya kimataifa.
Alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa karibu zaidi shirika limefungua ofisi za kanda saba (7) ambazo ni Mashariki, Kusini, Nyanda za juu Kusini, Ziwa, Magharibi, Kati na kasikazini.

Pia alisema pamoja na shirika kuthibidhisha ubora wa bidhaa, limekuwa likiwainua wajasiliamali wadogo katika kuthibitisha ubora wa bidhaa zao ili kuleta ushindani wa masoko na bidhaa nyingine kwa kutoa alama ya ubora kwao.
“Kama Shirika limetenga kiasi cha shilingi 250 milioni kwa mwaka kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadogo kuweza kuhakikisha bidhaa zao zinaweza kukidhi matakwa ya ubora,”alisema.
Alisema kutokana na wimbi la wajasiriamali wadogo na wabunifu wanaozalisha bidhaa kila siku kumekuwa na baadhi changamoto ikiwa ni kutofika ama kuuza bidhaa kinyemela bila kuwa na uthibitishwaji wa ubora kwani kwa kufanya hivyo wamekuwa wakivunja sheria ya viwango namba 2 ya mwaka 2009.
Kutokana na hilo alitoa wito kwa wajasiriamali hao kuepuka penati mbalimbali na kuwataka kutopeleka bidhaa zao sokoni kabla ya kuthibitishwa kwa ubora wa bidhaa zao na TBS, wanapopeleka bidhaa ambazo ziko kwenye viwango vya lazima kabla hazijakidhi matakwa ya ubora wanavunja sheria na kupelekea kuharibu biashara zao walizoanza nazo.

“Niwahimize kutumia ofisi za Sido na tovuti ya shirika ambapo wataelekezwa namna ya kufikia kiwango cha alama ya ubora kwenye bidhaa zao, na hiyo itaepuka hatari, na kwa sasa shirika limeondoa mirorongo kwa kuanzisha huduma ya kimtandao,” alisema.
Mfanyabiashara Maria Ayubu alisema kuthibitishwa kwa ubora wa bidhaa za wajasiriamali ni muhimu kwani inamfanya mtumiaji kuwa na uhakika na kwamba kwa sasa wanatambua umuhimu wa kuwa na alama ya TBS ambayo inasaidia kuondosha usumbufu wakati wa uuzaji wa bidhaa zao.
“Kimsingi elimu inatakiwa kuenelea kutolewa kwa wannchi hususani wajasiliamali, wafanyabiashara na hata wabunifu kwani bila kufanya hivyo bidha zisizokuwa na ubora zitaendelea kuzagaa maneo mengi na kuleta athari kwa watumiaji,”alisema Ayubu.