Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tembo Nickel yakabidhi miradi ya Sh208 milioni Ngara

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya msingi Nyabihanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakiwa wameketi ndani ya darasa na kwenye madawati yaliyotolewa na Kampuni ya Tembo Nickel kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii. Picha na Alodia Dominick.

Muktasari:

Miradi hiyo ya elimu na afya ambayo ni sehemu ya uwabikaji kwa jamii imekabidhiwa imekabidhiwa na Kampuni ya Tembo Nickel baada ya kukamilika kwa asilimia 100.

Ngara. Kampuni ya Tembo Nickel inayochimba madini ya Nickel wilayani Ngara imetekeleza na kukabidhi miradi 11 yenye thamani ya Sh208.11 milioni wilayani humo ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya kurejesha sehemu ya faida kwa jamii.

Akikabidhi miradi hiyo ya sekta ya elimu na afya iliyotekelezwa mwaka 2022, Meneja Mkuu wa Tembo Nickel, Manny Ramosh japo haijaanza uzalishaji, kampuni hiyo itaendelea kutekeleza miradi kama sehemu ya kuwajibika na kurejesha kwa jamii.

Miradi hiyo ya elimu na afya ambayo ni sehemu ya uwabikaji kwa jamii imekabidhiwa Kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mathias Kahabi leo Jumatano April 19, 2023 na Meneja Mkuu wa Tembo Nickel, Manny Ramosh.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika shule ya msingi Nyabihanga, Monash amesema utekelezaji wa miradi hiyo ya uwabikaji kwa jamii (CSR) unalenga kujenga mahusiano mema kati ya kampuni na jamii.

"Japo hatujaanza uzalishaji, mwaka jana Tembo Nickel tulisaini mkataba na Serikali mkataba wa kutekeleza miradi ya uwabikaji kwa jamii na yote tayari imekamilika kwa 100 asilimia. Hata mwaka huu tunatarajia kusaini mkataba mwingine wa kutekeleza miradi ya kijamii," amesema Monash

Mkuu wa Idara ya Mahusiano Kampuni ya Tembo Nickel, Chiza Patrick ametaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi Mukivumu, Ruhuba, Gwenzaza, Nyabihanga na Muganza.

Miradi mingine ni ujenzi wa ofisi za walimu na utoaji wa madawati zaidi ya 100 kwa shule za msingi, viti 80 na meza 80 kwa shule ya Sekondari Rulenge, ujenzi wa wodi ya wazazi na vifaa tiba katika Zahanati za Bugarama na Rwinyana pamoja na mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika vijiji tisa vya Wilaya ya Ngara.

Jasintha Buchwa, mkazi wa Bugarama ameishukuru kampuni hiyo kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi na ununizi wa vifaa tiba katika zahanati ya Bugarama akisema siyo tu imeboresha huduma, bali pia itaongeza mwamko wa akina mama wajawazito kujifungulia hospitalini.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mathias Kahabi amewaagiza viongozi wa vijijini na kata za wilaya hiyo kusimamia vema miradi hiyo iliyogharimu mamilioni ya fedha.