Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFS watakiwa kuendana na mabadiliko kijeshi

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa bodi ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS), Brigedia Jenerali Mbaraka Mkerermy, amewataka maofisa wa TFS waliopata mafunzo ya uongozi kuwa chachu ya kutatua changamoto na kuendana na mabadiliko ya kijeshi.

Arusha. Mwenyekiti wa bodi ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS), Brigedia Jenerali Mbaraka Mkerermy, amewataka maofisa wa TFS waliopata mafunzo ya uongozi kuwa chachu ya kutatua changamoto na kuendana na mabadiliko ya kijeshi.

Ameyasema hayo jana Januari 18, 2023 jijini Arusha katika halfa ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi kwa maofisa wa TFS kutoka makao makuu, vituo ikiwemo kanda za uhifadhi, mashamba ya miti, kituo cha mbegu na mashamba ya nyuki.

Amesema kuwa, utoaji wa mafunzo hayo ni mwendelezo wa maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, alipoitaka TFS kutekeleza mabadiliko ya utendaji kazi kutoka mfumo wa kiraia na kuwa mfumo wa kijeshi.

Amesema mabadiliko hayo yanayotekelezwa kwa mujibu wa sheria namba 2 ya mwaka 2020 iliyounda Jeshi la uhifadhi wa wanyamapori na misitu na amri zote kwa jumla.

"Mafunzo haya mara kwa mara yamewajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiutendaji na kuimarisha weledi katika utekelezaji wa shughuli zenu kwa mfumo mpya wa kijeshi, hivyo naombeni sana mkawe mabalozi kwa wengine katika maeneo yenu mnapofanyia kazi," amesema.

Ameongeza kuwa, maafisa hao wamefundishwa dhana mbalimbali za utekelezaji majukumu ya kijeshi ikiwemo masuala ya uongozi katika jeshi, masuala ya itifaki, operesheni za jeshi na intelijensia na matumizi ya mbinu fiche.

Mengine ni pamoja na mfumo wa mawasiliano na utoaji wa maelekezo ya kiutendaji, utekelezaji wa amri za jumla za jeshi na sheria za uhifadhi pamoja na kukumbushwa masuala ya gwaride na nidhamu ya jeshi.

Kwa upande wake, Kamishna wa uhifadhi wa wakala wa huduma za misitu, Profesa Dos Santos Silayo amesema katika utekelezaji wa mabadiliko kutoka mfumo wa kiraia na kuwa mfumo wa kijeshi, asilimia 98.6 watumishi wote wa TFS wamehudhuria mafunzo ya awali ya kijeshi.

Amesema baada ya kukamilisha mafunzo ya awali wameanza utekelezaji wa awamu nyingine inayolenga kujenga uwezo katika nyanja za uongozi na uperesheni za kijeshi.
Ameongeza utendaji kwa mfumo wa kijeshi wenye weledi unalenga kuiwezesha taasisi kutekeleza wajibu wake vizuri katika uhifadhi wa misitu na rasilimali nyuki ambazo ni kusimamia misitu yote ya hifadhi ya serikali ipatayo 463.

"Bado sekta hii inakabiliwa na changamoto zinazohitaji mbinu mpya za kijeshi za utatuzi ikiwemo uhaba wa watumishi jambo linalosababisha uvamizi wa misitu kwa shughuli za ufugaji na kufungua mashamba mapya na utafutaji wa kuni za kupikia," amesema.

Akizungumza awali, Naibu Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TFS, Emmanuel Kiboko amesema kuw wahitimu hao wapatao 47 wamejifunza mafunzo hayo ya uongozi ambayo yatasaidia kuinua na kuongeza weledi.