Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFS yapanda miti 500 kuokoa uoto Mto Nyamazugo

Muhifadhi wa Misitu wilayani Sengerema, James Aloyce akitoa maelenzo baada ya upandaji miti Kwenye chanzo cha maji Nyamazungo wilayani humo ikiwa ni Sehemu ya maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Picha na Daniel Makaka

Muktasari:

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imepanda miche ya miti 500 katika chanzo cha maji Nyamazugo ili kulinda uoto wake wa asili.

Sengerema. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imepanda miche ya miti 500 katika chanzo cha maji Nyamazugo ili kulinda uoto wake wa asili huku ikigawa mingine 134, 380 kwa wakazi wa wilaya hiyo pamoja na taasisi mbalimbali ili kutunza mazingira.

Miti hiyo iliyopandwa leo Jumatano Aprili 26, 2023 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 200 imepandwa katika chanzo hicho cha maji na 300 ikipandwa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Sengerema (Seuwasa).

Akizungumza wakati wa upandaji wa miche hiyo , Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Sengerema, Jemas Aloyce amesema wamegawa miche 134,380 ya matunda, mbao na kivuli kwa wananchi katika mwaka wa fedha 2022/23 ambayo imepandwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

“Tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida ya kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwamo vyanzo vya maji ili kutunza mazingira na kupata mvua za kutosha,” amesema Aloyce

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Aleni Agustine amezitaka taasisi za umma kutunza miti iliyopandwa kwenye maeneo yao katika maadhimisho hayo ili ikue na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Mkazi wa kata ya Nyamazugo, Amos John amesema elimu na hamasa ya upandaji miti na utunzaji mazingira inapaswa kuwa endelevu kwa wananchi kwani baadhi yao wamekuwa wakishindwa kuisimamia miti inayopandwa katika maeneo yao.

Diwani wa kata hiyo, Enock Sengerema ameipongeza TFS kwa kupanda miti katika chanzo cha maji Nyamazugo ili kukinusuru kisiharibike kwani hatua hiyo italinda uoto wa mto huo.