Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TLS: Mkataba wa bandari una ukinzani kisheria

Rais wa TLS, Harold Sungusia

Muktasari:

  • Chama cha Wanasheria Tanganyika kimebaini ukinzani wa kisheria katika mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji bandari ya Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) kimesema kimebaini ukinzani wa kisheria katika mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji na uboreshaji bandari ya Dar es Salaam kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World.

Kiini cha ukinzani huo, kwa mujibu wa TLS ni katika kifungu cha 21 cha mkataba huo kinachotaka sheria zitakazoongoza ni zile za Uingereza ilhali Serikali mwenyeji wa makubaliano ya mradi ni Tanzania.

Katika taarifa yake iliyoitoa leo, Juni 26, 2023 TLS imesema imebaini kifungu hicho kinasababisha mgongano wa kisheria kati ya pande zilizokubaliana.

“Ni vigumu mradi unatekelezwa Tanzania lakini ukaongozwa kwa sheria za Kiingereza,” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na hilo, TLS imependekeza marekebisho katika kifungu hicho, ikitaka sheria za Tanzania ndizo zitumike kuongoza mkataba huo.

“Hili linaweza kutekelezwa kupitia Kifungu cha 22 cha mkataba, mara baada ya uidhinishaji mchakato kukamilika ambapo mabadiliko ya vyombo vya uidhinishaji unafanyika kulingana na Kifungu cha 25(4),” imesema.

Imesema sheria ya Kiingereza na Tanzania zinatofautiana katika suala haki ya umiliki wa ardhi kwani ya Tanzania mgeni hawezi kumiliki ardhi kama inavyotakiwa na Sheria ya Ardhi ya Uingereza.

“Kulingana na sheria za Tanzania mgeni anamiliki ardhi kwa madhumuni ya uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),” imesema.

Pasi na kurekebishwa hilo, TLS inasema kutakuwa na mgongano wa sheria.