Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMB kuyafungia machinjio, minada 'bubu’ isiyokuwa na vibali

Ofisa Mifugo Mwandamizi, Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dk Mpoki Alinanuswe akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Septemba 27, 2023. Picha Hawa Mathias

Muktasari:

  • Lengo ni kudhibiti uanzishwaji holela na kudhibiti ubora wa nyama ili kulinda afya za walaji kutokana na baadhi ya maeneo  kuwa katika hali mbaya ya mazingira ikiwepo ukosefu wa huduma za vyoo na kwamba kati ya machinjio 10 mawili yamesajiliwa, huku minada nane iliyosajiliwa mawili pekee Jiji la Mbeya.

Mbeya. Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imesema itaanza zoezi la ukaguzi na kuyafungua machinjio na minada itakayobainika kutokuwa na vibali vya muda kwa lengo la kudhibiti uanzishwaji holela na ubora wa nyama.

Ofisa Mifugo Mwandamizi, kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dk Mpoki Alinanuswe ameiambia Mwananchi Digital leo Jumatano, Septemba 27, 2023 na kwamba lengo kuu ni kulinda afya za walaji na uanzishwaji holela wa makalo ya machinjio.

“Tumeanza kaguzi katika mikoa ya Njombe, Iringa na awali tumetoa muda wa usajili kwa machinjio zote ambazo hazitambuliki kisheria sambamba na kuagiza halmashauri zote kutekeleza hilo.”

Dk Alinanuswe amesema kwa Jiji la Mbeya kati ya  machinjio 10 mbili zina usajili  huku minada (magulio) yapo 8 yaliyosajiliwa ni mawili hali hiyo inaonyesha ni jinsi gani usimamizi unakuwa siyo mzuri jambo ambalo TMB imekuja na mpango huo ili kudhibiti usalama wa watumiaji wa kitoweo hicho na ubora wa nyama.

Amesema kuwa ukaguzi huo utafanywa Kanda nzima na baada ya hapo zipo ambazo zitafungiwa kabisa na nyingine kupata usajili wa muda pamoja na maelekezo ya uendeshaji.

“Kuna changamoto kubwa kwenye machinjio nyingi katika Jiji la Mbeya na minada kuwa katika hali mbaya ya usafi wa mazingira hususan huduma za vyoo ,sasa katika ufuatiliaji ni miongoni mwa maeneo yatakayositishiwa kutoa huduma.

Katika hatua nyingine, Dk Alinanuswe amesema kumekuwepo na kasumba ya watu hususan vijijini wanaweka wanajenga vibanda (machinjio bubu) na kuendesha shughuli za kuchinja mifugo jambo ambalo kisheria linakataliwa kwani kunahatarisha usalama wa afya za watumiaji kutokana na  kitoweo hicho kukosa ubora.

“Lengo la usajili na kutoa vibali vya muda ni kusaidia jamii kupata nyama iliyo bora na  inayokidhi vigezo sambamba kudhibiti machinjio na minada 'bubu'  ambapo pia tutafanya ukaguzi wa nyama zinazoingizwa buchani zinapimwa na madaktari wa mifugo na kuwa na mihuri ya utambulisho.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Ally Mbika amesema kuwa utaratibu wa uanzishwaji wa machinjio na minada itazamwe upya kwa kuzingatia mazingira rafiki ikiwepo upatikanaji wa huduma muhimu hususan matundu ya vyoo.


“Suala na miundombinu ya vyoo katika maeneo ya minada ni changamoto kubwa kwani ukosefu wa hudma hiyo kunaweza kuchangia magonjwa ya milipuko hususan kipindupindu kutokana na watu kujisaidia vichakani,”amesema.

Mfanyabiashara wa nyama choma Solomon Mwaisaka amesema utoaji wa vibali utasaidia kuwabana wachinjaji holela mitaani.

“Kuna changamoto ya mifugo kugonjwa au kuugua na kufa ambayo tumekuwa tukiletewa kuuziwa na baadhi ya wafugaji, pia tuombe tu kuwepo utaratibu wa ukaguzi wa nyama kwenye mabucha mara kwa mara ili kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu,”amesema.