Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMB yapiga marufuku matumizi ya magogo buchani

Ofisa mifugo Bodi ya Nyama Tanzania (TMB)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini , Dk Mpoki Alinanuswe akizungumzia changamoto na mafanikio ya sekta ya mifugo katika ofisi za gazeti hili. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Agizo hilo limetokewa leo Jumanne Juni 13, 2023  na Ofisa Mifugo Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Kanda ya Nyanda za Juu Kusin Dk Mpoki Alinanuswe  baada ya kubaini kuwepo baadhi ya wafanyabishara kuendelea kutumia magogo ya miti licha ya bodi kuelekeza matumizi ya vifaa vya kisasa.

Mbeya. Wafanyabiashara na wamikili wa maduka ya  nyama mikoa ya nyanda za juu kusini, wametakiwa kuzingatia  maagizo ya Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) kutumia vifaa maalum vya kukata nyama na kuachana na matumizi magogo ya miti ili kulinda afya za walaji.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 13,2023, Ofisa mifugo bodi ya nyama Kanda Dk Mpoki Alilanuswe amesema  tayari miongozo na maelekezo vilitolewa na kilichofuata ni utekelezaji na kwamba matumizi ya magogo ya miti yanaweza kuleta madhara kwa walaji wa mwisho.

“Sekta ya nyama ni sekta nyeti ambayo inahitaji umakini  mkubwa kuanzia hatua ya  uandaaji kutoka  kwenye machinjio  mpaka sokoni  sasa tunapotoa maelekezo lengo ni kuwepo kwa ubora wa kitowei hicho kwa walaji,”amesema.

Dk Alinanuswe amesema katika kukabiliana na hali hiyo bado wanaendela  kuhamasishaji matumizi ya vifaa vya kisasa kuandaa nyama, ikiwepo magogo ya plastiki wakati wa kukata kitoweo hicho kabla ya bodi kuanza kuchukua hatua za kufanya ukaguzi.

Wakati huo huo  ameomba Serikali na wadau kuwekeza nguvu kuboresha machinjio na uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kusindika nyama ili kusafirisha kupata  masoko ya nje ya nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA) .


“Nyanda za juu kusini kuna kiwanda kimoja cha usindikaji wa nyama ambacho asilimia kubwa wanategemea masoko ya ndani kutokana na kutokidhi vigezo vya kusafirisha nje ya nchi  hivyo kuna uhitaji wa nguvu ya serikali na wadau katika uwekezaji  kwani uhakika wa mifugo ni mkubwa ”amesema.

Mfanyabishara wa duka la nyama, Nassoro Nassoro amesema changamoto kubwa ya kufikia malengo ya utekeleza ni kutokana na baadhi yao kuwa na mitaji midogo ambapo matumizi ya vifaa vya kisasa  kucharangia nyama vinahitaji rasirimali fedha.

“Tunaomba Serikali itusaidie kupata mikopo ya vifaa hivyo ili tuweze kwenda na teknolijia za kisasa za uandaaji wa nyama kwa lengo la kulinda afya za walaji wa chini ,sambamba na kutenga maeneo maalum kwa ajili ya maduka  husika. ”amesema.

Mkazi wa Jijini Mbeya, Salome Joel ameiomba TMB kuweka msisitizo wa kupiga marufuku kutumia magogo ya miti kukata nyama kutokana na madhara kiafya kwani yamekuwa sio salama kutokana na kutofanyiwa usafi .