Tump: Tumefanya tulichokuja kufanya

Tump: Tumefanya tulichokuja kufanya

Muktasari:

  • Donald Trump leo Jumatano Januari 20, 2021 ndio siku anayoondoka Ikulu ya Marekani baada ya kuwa rais wa taifa hilo kwa miaka minne.

Marekani. Donald Trump leo Jumatano Januari 20, 2021 ndio siku anayoondoka Ikulu ya Marekani baada ya kuwa rais wa taifa hilo kwa miaka minne.

Katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2020, Trump alishindwa na mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biuden na kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo leo rais huyo mteule ndio anaapishwa.

Katika hotuba yake ya kuwaaga raia wa nchi hiyo, Trump amesema, “tumefanya kile ambacho tulikuja kukifanya na tumefanya mambo mengine mengi."

Katika video aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube amesema, “mapambano yalikuwa makali, vita ilikuwa ngumu kwa sababu hicho ndicho mlinichagua kukifanya.”

Trump anaondoka madarakani akiwa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kitendo ambacho kiliibua hali ya sintofahamu baada ya wafuasi wake kuandamana mara kadhaa kupinga ushindi wa Biden.

Wafuasi hao mapema mwaka 2021 walivamia jengo la Bunge la nchi hiyo wakipinga matokeo ya uchaguzi.

"Ghasia za kisiasa ni shambulio la kila kitu tunachothamini kama Wamarekani. Kamwe hatuwezi kuvumilia," amesema Trump  huku akisisitiza kutotambua ushindi wa Biden katika hotuba yake hiyo ya takribani dakika 20.

"Vita ilikuwa kubwa , mapambano yalikuwa makali  ni maamuzi magumu kwa sababu hiyo ndio sababu iliyowafanya mnichague," amesema Trump.