Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuzo za Tehama kufungua ajira, fursa za kimataifa kwa vijana

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania (ICTC), Dk Nkundwe Mwasaga, akizungumza leo Juni 17, 2026 wakati akitangaza tuzo za pili za Tehama za mwaka 2026, zitakazofanyika Jumatano Julai 15, 2026 Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Washindi wa mwaka jana walinufaika na mafunzo ya akili unde (AI) yaliyofanyika Dubai huku kampuni moja ikizalisha ajira zaidi ya 800.


Dar es Salaam. Tuzo za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) zinazotarajiwa kutolewa Julai mwaka huu 2026, zimeelezwa kuwa kichocheo muhimu cha ajira, ubunifu na fursa za kimataifa kwa vijana wa Kitanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatano Juni 17, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania (ICTC), Dk Nkundwe Mwasaga, amesema tuzo hizo zimekuwa zaidi ya jukwaa la kutambua ubunifu, bali njia ya kufungua fursa mpya katika uchumi wa kidijitali.

Dk Mwasaga Ameyasema hayo wakati akitangaza tuzo za pili za Tehama za mwaka 2026, zitakazofanyika Jumatano Julai 15, 2026 Dar es Salaam ambazo zimeandaliwa kwa ushirikiano kati ya ICTC, Kampuni ya SoftVenture Solutions na Chama cha Watoa Huduma za Intaneti Tanzania (Tispa).

Amesema mafanikio ya tuzo za mwaka 2025 yanaonesha mchango wake katika kukuza vipaji na ajira, akitolea mfano mshindi mmoja aliyepata fursa ya kwenda Dubai kusoma na kujifunza kuhusu akili unde (AI).

Aidha, amesema kampuni iliyoshinda tuzo mwaka jana ilifanikiwa kupata zabuni ya kuboresha maabara zaidi ya 200 za Tehama nchini, hatua iliyochangia kuzalishwa kwa ajira zaidi ya 800.

“Tuzo hizi zinalenga kutambua na kuthamini mchango wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya Tehama nchini, lakini pia kuhamasisha ubunifu unaoweza kuleta matokeo chanya kwa wananchi,” amesema Dk Mwasaga.

Amesema tuzo za mwaka huu zimegawanya katika makundi 14 ambayo yamejumuisha jumla ya makundi madogo 44 hadi kufikia hivi sasa, jumla ya maombi 345 yalikuwa yamepokelewa kwa ajili ya uchambuzi.

Amesema miongoni mwa vigezo vinavyozingatiwa ni ubunifu, ujumuishi wa kidijitali na uwezo wa miradi husika kuleta manufaa kwa jamii, ikiwemo kuongeza fursa za ajira.

Mkurugenzi Mkuu wa SoftVenture Solutions Company Limited, Caroline Kombe, amesema tuzo hizo zimeendelea kuimarisha ushindani na kuhamasisha maendeleo ya sekta ya Tehama nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha mauzo ya jumla wa kampuni ya YAS, Dk Yvonne Mashuda, amesema taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za kuibua vipaji vya Watanzania na kukuza ujumuishi wa kidijitali.