Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twitter yataka programu ya Threads isitishwe, yatuma barua Meta

Twitter yavurugwa Nigeria, yatetewa

Dar es Salaam. Baada ya Meta kuzindua programu ya Threads ambayo imepata umaarufu na hivyo kusajili watumiaji 30 milioni ndani muda mfupi tangu kuziunduliwa kwake, Twitter imeitumia barua Meta ikiitaka kusitisha na kuachana na programu hiyo.

Hii ni kwa mujibu mtandao wa ‘ABC News’ ambao umesema vyanzo vyenye ufahamu juu ya barua hiyo, vimeiambia television hiyo kwamba barua hiyo ilitumwa na timu ya wanasheria ya Twitter Jumatano Julai 5, 2023.

Barua hiyo imeishutumu Meta kwa kutumia vibaya siri za biashara za Twitter na kwamba ili kufanikisha azma yake Meta iliajiri wafanyakazi wa zamani wa Twitter ambao kwa asili ya kazi zao, wameendelea kuwa na ufahamu wa taarifa za hakimiliki, vyanzo hivyo vimeeleza.

"Katika mwaka uliopita, Meta imeajiri wafanyakazi kadhaa wa zamani wa Twitter," barua hiyo, ambayo imesainiwa na wakili Alex Spiro, inasomeka. "Twitter inajua kuwa hapo awali, wafanyakazi hawa walifanya kazi Twitter; kwamba wafanyakazi hawa walikuwa na wanaendelea kupata siri za biashara za Twitter na taarifa zingine za siri za ndani; kwamba wafanyakazi hawa wana deni la kuendelea kuwa waaminifu kwa Twitter; na kwamba wengi wa wafanyakazi hawa wamehifadhi isivyofaa nyaraka na vifaa vya kieletroniki vya Twitter.”

Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa: "Kwa ufahamu huo, Meta iliwapa kazi wafanyakazi hao kwa makusudi, katika muda wa miezi kadhaa ili watengeneze programu ya Meta ya "Threads" kwa kutumia siri za biashara za Twitter na hakimiliki nyingine, na hivyo kuharakisha utengenezwaji wa programu hiyo shindani, kitu ambacho ni ukiukwaji wa sheria za jimbo na nchi kwa ujumla, lakini pia ni kinyume na wajibu wao wa uaminifu endelevu kwa Twitter."

Katika juhudi zake za kupunguza gharama za uendeshaji kwa kiasi kikubwa, Kampuni ya Twitter ilipunguza takriban asilimia 75 ya wafanyakazi wake 7,500 muda mfupi baada ya Elon Musk kuinunua kampuni mwaka jana.

Akijibu ujumbe mfupi kwenye uliotumwa kwenye Twitter kuhusu barua hiyo ya kuitaka Meta ya kusitisha na kuacha kuendelea na programu hiyo, Musk amesema: "Ushindani ni sawa, lakini kudanganya siyo sawa."

Yakionekana kama ni majibu yasiyo rasmi kuhusu barua hiyo, Msemaji wa Meta, Andy Stone, ameandika kwenye Threads akisema: "Hakuna mtu kwenye timu ya uhandisi ya Threads ambaye amewahi kuwa mfanyakazi wa Twitter."

Mtandao wa Threads, ambao umetengenezwa kutoka kwa programu iliyopo kwenye mtandao wa Instagram, umekuwa maarufu sana katika saa zake 24 za kwanza tangu kuzinduliwa kwake hapo jana Julai 6 2023 muda wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Meta Mark Zuckerberg alisema siku ya Alhamisi asubuhi kwamba programu hiyo tayari imesajili watumiaji milioni 30.