Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ugonjwa wa polio bado tatizo Pakistan

Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa, imeripotiwa kuwa ugonjwa wa polio umeendelea kulitesa Taifa la Pakistan.

Taarifa za vyombo mbalimbali vya habari nchini humo zinaeleza kuwa mwaka jana zimeripotiwa kesi zaidi ya 68 ikilinganishwa na nchini Afghanistan ambako watoto 25 waliougua ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Mpango wa Kutokomeza Polio Duniani (GPEI), mapambano ya kutokomeza ugonjwa huo yamekuwa ya mafanikio na kesi zimeshuhudiwa kupungua kwa asilimia kubwa lakini hali imekuwa tofauti nchini Pakistan na Afghanistan.

Pia, mwaka 2023 Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kupungua kwa ugonjwa huo lakini Pakistan na Afghanistan zimeendelea kutajwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

‘’Kushindwa kwa Pakistan kuondoa polio ni kutokana na kukosekana kwa chanjo ya ugonjwa huo, kukosekana kwa ufadhili wa mataifa mbalimbali na nchi kutokuwa na utulivu wa kisiasa  pamoja na kukosa mfumo mzuri wa huduma za afya.’’

‘’Hapa Pakistan kumekuwa na tatizo moja kubwa, baadhi ya wananchi wanatilia shaka chanjo zinazoletwa, kuna tetesi kuwa chanjo zina madhala na hili linazungumzwa sana kwenye mitandao ya kijamii, nadhani elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi,’’ alieleza mmoja wa wanaharakati nchini humo kwa sharti la kutotajwa jina wakati akihojiwa na mitandao wa Dawn.

Habari zaidi zinaeleza kuwa juhudi za usambazaji wa chanjo, mapambano dhidi ya ugonjwa huo yanakwamishwa na mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo.

‘’Kuna baadhi ya maeneo wahudumu wa afya wanauawa na hawa wanamgambo, sasa hapo ukichangia na uratibu usiokidhi viwango ni wazi kuwa hali haiwezi kuwa kama inavyotarajiwa,’’ alinukuliwa mmoja wa wanaharakati katika mitandao wa Dawn.