Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukame waua mifugo 1,257 Kilimanjaro

Muktasari:

  • Mifugo 1,257 imekufaa mkoani Kilimanjaro kutokana kukosa maji na malisho baada ya ukame kukumba eneo hilo.


Moshi. Mifugo 1,257 imekufaa mkoani Kilimanjaro kutokana kukosa maji na malisho baada ya ukame kukumba eneo hilo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo mkoani humo kwa ajili ya kuzindua Tamasha la Utamaduni.

Kagaigai ametaja mifugo hiyo iliyokufa kuwa ni ng’ombe 841, kondoo 406 na punda 10

"Mweshimiwa Rais, pamoja na mafanikio na kazi mbalimbali za maendeleo zinazoendelea, Mkoa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutonyesha kwa mvua za vuli, hali ambayo imesababisha ukame na vifo vya mifugo.

" Uongozi wa mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na hali hiyo. Pamoja na vifo hivyo vya mifugo, hali ya chakula bado ni nzuri, na Mkoa unachakula cha kutosha” amesema Kagaigai.