Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukatili kwa watoto janga la Taifa

Naibu Katibu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Amon Mpanju.

Dodoma. Serikali imesema kuwa, ukatili wa watoto janga kwa Taifa ambalo lazima kukivalia njuga kwenye mapambano.

 Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Julai 24,2024 na Naibu Katibu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Amon Mpanju aliyesema chanzo cha ni mmomonyoko wa maadili.

Mpanju alikuwa akifungua kikao cha Makatibu Wakuu kwa pande mbili za Muungano kuhusu utafiti wa ustawi, afya ya watoto na vijana ambacho kimefanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu amesema kila mwaka matukio ya ukatili wa watoto yamekuwa yakiongezeka kila wakati huku ubakaji likitajwa janga linaloongoza zaidi katika matukio hayo.

Amesema kwa mwaka 2022 pekee jumla ya watoto 12,163 walifanyiwa ukatili na kati ya hao 6,365 ilikuwa ni matukio ya ubakaji.

"Kwa hiyo lazima tuje na utafiti wenye kuleta suluhisho, maana kuna ukatili mkubwa tena kwenye mitandao na haya yote yanatokana na mmomonyoko wa maadili," amesema Mpanju.

Ameagiza utafiti unaokwenda kufanyika ukawe wenye tija na kuwashirikisha walengwa akasisitiza njia sahihi iwe ni kusaidia kuondoa maumivu kwa watoto.

Hata hivyo Mpanju amesema haridhishwi na neno 'makundi maalumu' kwani linatumiwa vibaya na watu hivyo utafiti utaje kama ni wenye ulemavu au shida nyingine kuliko kujificha kwenye neno makundi maalumu.

Kwa mujibu wa Mpanju, utafiti huo utaanza mapema iwezekanvyo baada kupitishwa kwa kikosi kazi leo ambacho kimejaa wabobezi na watashirikiana na taasisi zisizo za kiserikali kwa ufadhili wa watu wa Marekani.

Kwa mara ya mwisho Tanzania ilifanya utafiti kama huo mwaka 2009 ambao ulikuja na majibu yaliyopelekea kutungwa kwa sheria ya ambayo kila upande wa Muungano walitunga.