Unachopaswa kufahamu kuhusu Siku ya Taifa la Ufaransa

Muktasari:

  • Bastille” ni neno linalotumiwa na nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza kurejelea “Siku ya Taifa la Ufaransa”, ambayo huadhimishwa kila Julai 14 ya kila mwaka. Huko Ufaransa siku hii inatambulika kama “Fête nationale; Maadhimisho ya Kitaifa” na kwa kawaida na kisheria hufahamika kama “Le 14 juillet” kwa Kifaransa (Julai 14 kwa Kiswahili).

Bastille” ni neno linalotumiwa na nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza kurejelea “Siku ya Taifa la Ufaransa”, ambayo huadhimishwa kila Julai 14 ya kila mwaka. Huko Ufaransa siku hii inatambulika kama “Fête nationale; Maadhimisho ya Kitaifa” na kwa kawaida na kisheria hufahamika kama “Le 14 juillet” kwa Kifaransa (Julai 14 kwa Kiswahili).

Asili ya siku hii inaanzia nyuma kidogo, kulipotokea uvamizi katika gereza maarufu la wakazi wa jiji la Par-is, Bastille, Julai 14, 1789, na hapo ndipo kilipokuwa kiini cha harakati za Mapinduzi ya Ufaransa.

Baadaye sherehe hizi ziliunganishwa na kuadhimishwa kwa pamoja na zile za Fête de la Fédération, zikisheherekea umoja wa watu wa Ufaransa Julai 14, 1970. Sherehe za Bastille hufanyika ndani ya Ufaransa yote.

Gwaride kongwe na kubwa huitishwa aghalabu ndani ya Ulaya asubuhi ya Julai 14, katika mtaa/eneo la Champs-Élysées lililopo Paris, mbele ya Rais wa Ufaransa, sambamba na maofisa wengine na wageni waalikwa. Siku hiyo ndiyo iliyoasisi demokrasia ya serikali ya Jamhuri na kuhitimisha utawala wa kidhalimu.

 Yafuatayo ni mambo ya msingi unayohitaji kuyafa-hamu kuhusiana na kwa nini siku hii ni kubwa na inasheherekewa.

Uvamizi wa gereza la Bastille

Tukio hilo lilitokea Julai 14, 1789 kufuatia mtikisiko mkubwa wa kiuchumi na kisiasa, huku mtawala wa mabavu aliyeshindikana, Louis XVI akishindwa kuyadhibiti makundi ya wanamgambo yaliyokuwa yakipinga utawala wake wa kidhalimu.

Bastille, ni ngome ya zama za mawe za kati na gereza, lilikuwa ni alama ya utawala wa kidhalimu wa Bourbon katikati ya mji wa Paris na ambaye aliwashikilia wakosoaji wake wa kisiasa.

Baada ya muda wa majadiliano kupita ikichagizwa na hasira walizokuwa nazo watu, makundi ya watu wapatao 1,000 walivunja ngome na gereza hilo na kufanikiwa kuingia ndani. Kufuatia masaa kadhaa ya mapigano, makundi hayo yaliweza kuchukua eneo hilo huku mlinzi mmoja na wapiganaji wao wapatao 100 wakijeruhiwa.

Sherehe za Umoja wa Ufaransa (Fête de la Fédération)

Mapema 1789, mwaka wa uvamizi wa gereza la Bastille, taratibu za awali za uandaaji muundo wa tamasha la kitaifa zilikuwa zikiendelea. Miundo hii ilikusudiwa kuimarisha utambulisho wa kitaifa wa nchi kupitia maadhimisho ya matukio ya Julai 14, 1789.

Moja ya miundo ya kwanza iliyopendekezwa na Clément Gonchon, mfanyakazi wa kiwanda cha nguo wa Ufaransa, ambaye aliwasilisha muundo wake wa sherehe ya kuadhimisha kumbukizi ya uvamizi wa gereza la Bastille kwa uongozi wa jiji huko Ufaransa na umma Desemba 9, 1789.

Kulikuwa na mapendekezo mengine na sherehe zisizo rasmi za Julai 14, 1789, lakini shere-he rasmi zilizowezeshwa na Bunge la Kitaifa ziliitwa “Fête de la Fédération” kwa maana ya “Sherehe za Umoja wa Kitaifa”. Fête de la Fédération Julai 14, 1790 zilikuwa ni sherehe za umoja wa taifa la Ufaransa wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa.

Lengo la sherehe hizi, mwaka mmoja baada ya tukio la uvamizi wa Bastille, ilikuwa kuashiria amani. Hafla hiyo ilifanyika katika eneo la Champ de Mars, ambalo kwa muda huo lilikuwa mbali kidogo ya jiji la Paris.

Kwa nini siku hii ni muhimu?

Siku hii imekuwa ni sababu ya kusambaa kwa kasi harakati za mapinduzi na baadaye kushuhudia uon-dolewaji madarakani kwa utawala wa Bourbon na kunyongwa kwa Louis XVI sambamba na mkewe, Malkia Marie Antoinette. Gereza hilo lilivunjiliwa mbali ndani ya miezi mitano tu na kilichobakia kwa sasa ni sanamu pekee katika eneo hilo.

Kwa nini Wafaransa wanasherehekea leo?

Wafaransa wanasherehekea alama zote kuu zin-azowakilisha taifa lao kama vile; bendera ya taifa yenye rangi tatu na wimbo wa taifa, vyote chimbuko lake likiwa ni Mapinduzi hayo.

Licha ya kusherehekea uvamizi wa gereza la Bastille pekee, lakini hii pia ni siku ya misingi mikuu mitatu ya Jamhuri yao ya “Uhuru, Usawa na Udugu” Ni ufahari wa kizalendo zaidi kuliko historia ya kisiasa ndiyo msingi wa leo.

Inasherehekewaje?

Ni sikukuu ya Kiserikali huko Ufaransa, husherehek-ewa kwa upigwaji wa baruti angani, chakula cha pamoja na magwaride. Gwaride hupita katika mtaa wa Champs-Élysées kutokea Arc de Triomphe hadi Place de la Concorde, ambapo Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, serikali yake na mabalozi kutoka nchi zingine nchini Ufaransa husimama.

Hili ni tukio kubwa na maarufu Ufaransa, ambalo hurushwa katika Televisheni ya Taifa ya Ufaransa na ndilo gwaride kongwe na kubwa la kijeshi kwa Ulaya.