Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unajisikia uchovu wa mwili mara kwa mara, huenda unasumbuliwa na maradhi haya

Muktasari:

  • Lakini je? Vipi kwa upande wa mtu yule ambaye anahisi uchovu uliokithiri tena wa mara kwa mara tofauti na kiasi cha kazi iliyoutumikisha mwili wake au akili yake?

Kila mwanadamu hupitia hali hii na hasa baada ya shughuli mbalimbali ambazo zilitumia nguvu au akili. Ni rahisi kutambua sababu zinazosababisha uchovu na hasa wa miili kutokana na shughuli zetu za kila siku.

Lakini je? Vipi kwa upande wa mtu yule ambaye anahisi uchovu uliokithiri tena wa mara kwa mara tofauti na kiasi cha kazi iliyoutumikisha mwili wake au akili yake?

Hili ni swali linalowasumbua wengi. Leo nitakueleza msomaji wangu wa safu hii sababu kuu zinazosababisha uchovu wa mara kwa mara tena ule uliokithiri ambao wakati mwingine sababu yake haiwezi kutambulika kwa haraka.

Aidha naomba nikukumbushe msomaji kwamba, sababu hizi ninazozieleza ndizo zinazosababisha uchovu kwa kiasi kikubwa. Lakini pia wakati mwingine uchovu husababishwa na matatizo mengine ya kiafya. Hivyo ni vyema kuwaona wahudumu wa afya kwa vipimo ikiwa haupo kwenye sababu hizi laki bado unapata uchovu wa mara kwa mara

Kitu cha kwanza kinachobabisha uchovu uliokithiri ni kukosa muda wa kutosha wa kupata usingizi. Kiafya mwanadamu anashauriwa kupata muda kadhaa wa kulala na kuweza kupumzisha akili na muda huu hutofautiana kati ya umri na umri ambapo watoto wenye umri wa miaka 0-3 wanatakiwa kulala kwa saa 14 hadi 17 kwa siku.

Muda huu hupungua taratibu kadri mtu anavyokua na kuongezeka umri ambapo kwa watoto wa umri wa miaka 4-17 kiafya wanatakiwa kulala kwa muda usiopungua saa 10 lakini wale wa umri wa kuanzia miaka 18 hadi miaka ya kukaribia 60 wanashauriwa kulala kwa muda wa saa zisizopungua 8.

Muda wa kulala pia unaongezeka kadri mtu anavyozeeka kuanzia miaka 60 na kuendelea. Hivyo vi vyema kutambua kiasi cha muda stahiki unaopaswa kulala kulingana na umri wako. Kinyume na hapo tatizo la uchovu wa mara kwa mara linaweza kuwa la kudumu kwako.

Aidha nashauri ni vyema kuacha kutumia vihatarishi vinavyoathiri mfumo wa akili na kusababisha mtu kushindwa kupata usingizi wa kutosha kama vile uvutaji wa sigara, bangi na vitendo vya ulevi kwa ujumla na kuacha unywaji wa vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa na vinywaji vya kiwandani vya kuongeza nguvu.

Mlo pia ni moja ya sababu zinazochangia uchovu. Watu wengi hawajui kama aina ya  chakula kinaweza kuwa sababu ya uchovu. Ndio maana inashauriwa kula mlo kamili wakati wote lakini sio mlo kamili tu lakini pia kula kwa wakati na kiasi stahiki cha ulaji.

Kutokula kiasi cha kutosha cha chakula kinaweza kumfanya mto kuhisi njaa na kupata uchovu. Lakini kwa upande wa pili, ulaji wa kupita kiasi sio tu hatari kwa afya lakini pia kunasababisha uchovu na hasa kama mtu akishiba kupita kiasi au kuvimbiwa kama ilivyozoeleka.

Na hapa kwenye mlo pia nashauri kunywa maji ya kutosha. Mwili ukikosa kiwango stahiki cha maji mwili hukosa nguvu na kuwa mchovu. Katika toleo lijalo nitaendelea kukueleza sababu zaidi zilizopo nyuma ya uchovu uliokithiri. Usikose nakala yako.

Kitu kingine ambacho huenda hukuwahi kukifikiria kama kingeweza kuwa chanzo kikubwa cha uchovu uliokithiri ni sababu za kisaikolojia. Hapa namaanisha matatizo kama msongo wa mawazo na sonona.

Ni kawaida kuwa na mawazo ya hapana pale lakini mawazo yakizidi yanakua adui kwa afya ya akili na hata mwili kwa ujumla na kwa upande wa mwilini, mara nyingi sana kuwaza kupita kiasi kunaweza kusababisha hali ya homa na uchovu wa mwili uliopitiliza.