Unesco yapiga ‘tafu’ sekta ya habari nchini

Dar es Salaam. Serikali imesaini makubaliano ya miaka mitano na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu, sayansi na utamaduni (Unesco) kwa ajili ya kuimarisha uchumi, ujuzi na usalama wa wanahabari.

Makubaliano hayo ambayo yamesainiwa leo Juni 3, 2023 jijini Dar es Salaam kati ya Waziri mwenye dhamana, Nape Nnauye na Mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini Tanzania, Michel Toto, ni hatua njema na inayoungwa mkono na wadau wa habari nchini.

Kwa upande wa Waziri Nape, ametaja maeneo mengine ya kunufaika ni pamoja na uimarishaji wa mazingira ya kisera na kisera, mfunzo kwa wanahabari, kuimarisha mifumo ya kidigitali.

“Ushirikiano huu utakuwa na mchango mkubwa sana sekta ya habari, utasaidia eneo la uchumi wa vyombo vya habari, lakini hata ulinzi na usalama kwa waandishi,” amesema Nape.

Toto amesema makubaliano hayo yanayotekelezwa kama sehemu ya mkakati wa ushirikiano wa 2022/27 kati ya Serikali na Unesco.