Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usafiri kivuko cha MV Kitunda Lindi warejea

Kivuko cha MV Kitunda kikiwa tayari safari baada ya kusimama kwa siku 14 kutokana na hitilafu. Picha na Bahati Mwatesa

Muktasari:

  • Mei 22, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack aliuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), kuhakikisha usafiri wa kivuko cha MV Kitunda unarejea ndani ya siku 14.

Lindi. Siku 18 baada ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack kutoa maagizo ya kusimamishwa kivuko cha MV Kitunda kutokana na hitilafu, kivuko hicho sasa kimeanza kazi.

Mei 22, 2024, RC Telack aliuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa) kurejesha huduma ya usafiri ndani ya siku 14.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa Juni 7, 2024, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga,  amesema kuwa Kivuko cha MV Kitunda kimeanza kufanya safari zake baada ya hitilafu iliyokuwepo kutengenezwa.

Ndemanga amesema pamoja na kujiridhisha na usalama wa kivuko hicho, amewataka wahandisi wote wasiondoke ili waweze kukiangalia mwenendo wake.

"Baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa nilitoka mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama kwenda kukagua na nikajiridhisha na kuwataka wahandisi wote waliofanya marekebisho ya kivuko hicho wasiondoke ili kuangalia ndani ya siku hizi hali itakuaje," amesema Ndemanga.

"Kwa kuwa kivuko hiki sio kipya, kinatakiwa matengenezo mara kwa mara, mkuu wa mkoa ameagiza mhandisi wa Temesa pamoja na mhandisi wa kampuni ya DMG kutoondoka mapema na kukaa kuangalia mwenendo wa kivuko hicho," amesema.

Licha ya kuanza kuvusha kivuko hicho, baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika muda mrefu wanaokaa kusuburi kuvuka hali ambayo imekuwa ikiwakera na kuwapotezea muda.

Zuberi Abdul aliyekuwa akisafiri kutoka Lindi mjini kuelekea Kitunda, amesema kuwa awali walikuwa wanasubiri kivuko nusu saa wanavuka, lakini sasa wamekuwa wakisubiri hadi saa mbili ndipo waanze safari.

"Yaani hapa tunakaa zaidi ya saa mbili kusubiri kuvuka, awali tulikuwa tunakaa nusu saa, ukija huku upande wa mjini nusu saa na upande wa Kitunda nusu saa, lakini sasa hivi ukienda upande wa Kitunda unakaa ukija huku unakaa zaidi ya saa moja wakati mwingine hadi saa mbili imekuwa kero sana kwa kuwa tunapoteza muda mwingi kusubiri kuvuka," amesema Zuberi.

Naye Emoso Juma mwanafunzi wa Sekondari ya Angaza,  amesema kuwa muda mwingi ambao wanaupoteza kukaa kusubiri kivuko kurudi nyumbani wanachelewa kufua nguo za shule pamoja na kufanya kazi nyingine.

"Tunamuonba mkuu wa mkoa atusaidie kuingilia kati suala la muda, warudishe kama zamani kwa sasa hivi imekuwa kero sana hasa kwa wanafunzi tunaosoma huku mjini," amesema Emoso.