Ushirikiano katika suala la elimu ya juu kati ya Ufaransa na Tanzania unashamiri

Wednesday July 14 2021
elimupic

Ukiwa umejikita zaidi katika kada ya lugha pekee kwa muda mrefu, Ushirikiano wa Elimu ya Juu kati ya Ufaransa na Tanzania umetanua wigo tangu mwaka 2019 kwa kuongeza kada zingine hususan zile za sayansi.

 Ushirikiano wa kitaasisi kati ya nchi hizi mbili huruhusu sasa taasisi kufanya baadhi ya mambo kwa pamoja kuhamasisha mabadilishano ya wanafunzi na vitivo, utafiti wa pamoja, usimamizi wa tafiti, shahada mbili na msaada wa kujifunza Kifaransa.

Mwaka 2019, Maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Juu ya Tanzania na Ufaransa yalifanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha maafisa wa vyuo vikuu na kujadili njia zinazowezekana za ushirikiano ili kuchochea ubadilishanaji wa masuala ya kitaaluma, miradi ya pamoja ya tafiti na maarifa.

Maonyesho ya pili ya Elimu ya Juu ya Tanzania na Ufaransa yatafanyika mwanzoni mwa mwaka 2022.

Taasisi nyingi za Ufaransa tangu wakati huo aidha zimeonyesha nia yao au zimetembelea Tanzania ili kuanzisha uhusiano na kujenga ushirikiano. Hizi ni pamoja na: Shule za Biashara na Uhandisi za Paris, Vyuo Vikuu vya Bordeaux, Aix Marseille na Grenoble.

Tanzania na Ufaransa hushughulikia athari za kiafya za dawa za waduduIli kutoa mfano thabiti wa ushirikiano kama huo kati ya Vyuo Vikuu vya Tanzania na Ufaransa, mwaka huu Ubalozi wa Ufaransa umekuwa ukisaidia mpango mpya wa utafiti unaojikita kushughulika na athari za kiafya za dawa za wadudu nchini Tanzania na zaidi barani Afrika.

Advertisement

Lengo ni kuziibua athari hasi za dawa za wadudu kwa afya ya binadamu ili kuijulisha na kuishauri vizuri Serikali ya Tanzania. Sehemu hii ya utafiti imeshika kasi barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ongezeko la matumizi ya dawa za wadudu katika kilimo cha kawaida.

 “Kemikali zinazoaminika kuwa hatari, zinazotumiwa kupambana na wadudu na kudaiwa kui-marisha uzalishaji, ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira. Kutafiti kiwango cha madhara ni muhimu ili kufahamisha watun-ga sera na hatua ziweze kuchu-kuliwa,” alisema Dk Vera Ngowi, Mchunguzi Mkuu na Mratibu wa mpango huo.

Mpango huo unajumuisha vituo vya utafiti kutoka nchi mbalimbali kama vile; Ivory Coast, Burkina-Faso, Ufaransa, Ujerumani, Norway na Marekani. Watafiti zaidi ya 30 wamejitolea kushiriki katika mpango huu uliounganisha kada mbalimbali, ambao unaweza kuwa hatua ya kwanza kuelekea katika ushirikiano wa kisayansi wa kimataifa wa muda mrefu katika athari za kiafya zinazohusiana na matumizi ya dawa za wadudu.

 “Madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya dawa ya wadudu ni jambo linalogusa watu wengi hapa nchini, lakini uandikaji wa taarifa athari hizi kisayansi ni jambo gumu. Tanzania ni moja wapo ya nchi chache za Kiafrika ambazo wanasayansi wachache wamefanya tafiti za hali ya juu ya suala hili. Ni furaha na heshima kufanya nao kazi ”anasema Dk Moritz Hunsmann (CNRS, kituo cha utafiti cha Ufaransa).

Advertisement