Ushirikiano wa MeTL na Panasonic kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za umeme kwa Watanzania

Mkurugenzi Mtendaji-Operesheni wa MeTL, Indrabhuwan Kumar Singh (kushoto), Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji (katikati), Mkuu wa Biashara na Mauzo wa Panasonic Life Solution India, Vishal Nangalia San (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi (Afrika Mshariki na Kati) Panasonic life solution India, Pradul Gangrude (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja n baada ya kutangaza ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni hizo.



Muktasari:

“Chapa ya Watu” (The peo­ple’s brand) ndivyo unavyoweza kuiita kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) kutokana na kugusa na kubadili maisha ya maelfu ya watu Tanzania na Afrika kwa ujumla.

“Chapa ya Watu” (The peo­ple’s brand) ndivyo unavyoweza kuiita kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) kutokana na kugusa na kubadili maisha ya maelfu ya watu Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kampuni hiyo ambayo inaon­goza kwa uzalishaji na usamba­zaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kwa miaka mingi imegusa na kubadili mai­sha ya watu kwenye nchi za; Malawi, Mozambique, Uganda, Zambia, Congo DRC, Rwanda, Tanzania, Ethiopia na Burundi.

Septemba 7 mwaka huu kam­puni hiyo iliingia makubaliano na kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya umeme ya Panasonic Life Solution India.

Makubaliano hayo yanaifanya kampuni ya MeTL kuwa msam­bazaji mkuu aliyeidhinishwa wa bidhaa za Panasonic Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya kuingia makubaliano hayo , Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji amesema wamekuwa wakifanya juu chini kukamilisha makubaliano hayo kwa miezi kadhaa iliyopita ili kuweza kufika hapo na kuwa tayari kusonga mbele na ush­irikiano huo mpya.

“Biashara zetu zote mbili zinaamini katika kutengeneza ulimwengu bora kwa wateja wake. Panasonic inasimamia “Maisha bora, ulimwengu bora” na sisi MeTL tunasema “Tunagusa maisha yako” hakika muungano huu umekamilika na uko tayari kutoa masuluhisho bora ya upatikanaji wa vifaa vya umeme kwa Watanzania,” amesema Fatema.

Amesema MeTL itakuwa msambazaji pekee na mkubwa aliyeidhinishwa na Panasonic Life Solution India hapa nchini ambapo bidhaa mbalimbali kama vile; swichi, soketi na feni zenye chapa ya Panasonic zitakuwa zinaingizwa nchini na kusambazwa na kampuni ya MeTL. “Kuna msemo unasema “ukitaka kwenda haraka nenda peke yako, ukitaka kwenda mba­li nenda na wenzako”, hivyo kwa kuzingatia ukubwa na ubora wa kampuni hizi mbili ushirikiano huu utatufikisha mbali na uta­saidia upatikanaji wa bidhaa za umeme zenye ubora na uhaki­ka kwa wananchi,” amesema Fatema.

Fatema amesema idara ya masoko ya kampuni hiyo ime­jipanga kuhakikisha bidhaa za Panasonic zinawafikia na kuku­baliwa na zaidi ya ilivyo sasa.

“Sisi idara ya masoko ya MeTL kwa kushirikiana na idara ya masoko ya Panasonic tutafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha bidhaa hizi zinawafikia walaji kwa urahisi, unafuu, ubora na haraka,” amesema Fatema.

Amesema kabla ya kuingia makubaliano hayo wamefanya utafiti kuangalia mahitaji ya vifaa vya umeme na wamegun­dua kuwa kuna uhitaji mkubwa wa upatikanaji wa uhakika, ura­hisi na ubora wa vifaa hivyo.

Fatema alihitimisha kwa kui­shukuru Panasonic Life Solution India kwa kuiyamini MeTL kuwa mshirika wake wa kibiashara hapa nchini na kueleza kuwa watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo kuiishi imani hiyo.

Mkurugenzi wa Mauzo wa MeTL, Hussein Dewji amesema ushirikiano huo ni wa kihistoria hapa nchini na wao kama idara ya mauzo watahakikisha upati­kanaji wa bidhaa za Panasonic unakuwa wa uhakika katika mikoa yote Tanzania.

“Tunayo timu imara kwa ajili ya kufanya matangazo na mauzo ya bidhaa za Panasonic kwe­nye soko la Tanzania. Hivyo tutafanya kazi kwa nguvu ili kuhakikisha tunafanikisha hili,” amsema Dewji.

Amesema MeTL inazalisha bidhaa nyingi ambazo zime­kuwa sehemu ya maisha ya watu hivyo kwa kutumia uzoefu huo watahakikisha bidhaa za Pana­sonic zinawafikia Watanzania wengi.

“Changamoto kubwa ya soko la bidhaa za umeme ni baadhi ya watu wasio waaminifu kuuza bidhaa zisizo na ubora jambo linaloleta shida kwa wanan­chi, hivyo tutahakikisha watu wanapata bidhaa bora na halisi za Panasonic ambazo zimeto­ka moja kwa moja wazalishaji wenyewe,” amesema Dewji.

Mkuu wa Biashara na Mau­zo wa Panasonic Life Solution India, Vishal Nangalia San ame­sema wana furaha kushirikiana na MeTL kwa sababu ni kampuni inayoongoza sekta ya biashara ya Afrika Mashariki hivyo bid­haa zao zitakuwa na uhakika wa soko kubwa.

“Moja ya sababu zilizochan­gia kuichagua kushirikiana na MeTL ni kutokana na ubora wa bidhaa zake ambao umewajen­gea imani kubwa kwa walaji. Pia ni kampuni ambayo inagusa maisha ya watu wengi hivyo tunatazamia nyakati za kusi­simua zaidi kutokana na ush­irikiano huu,” amesema Vishal.

Vishal amesema wanaamini kuboresha maisha ya watu kwa kutumia bidhaa zao hivyo kwa kuungana na MeTL ambao nao wamewekeza katika kugusa na kubadili maisha ya watu ush­irikiano huo utakuwa na manu­faa makubwa kwa watumiaji wa bidhaa za Panasonic.