Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utambuzi wanavyovuna mamilioni kwa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa

Muktasari:

Uhakika wa kuuza zaidi ya lita 4500 za maziwa kila siku kumewafanya wafugaji wa chama cha Ushirika cha Utambuzi 

Mbeya. Wakati wafugaji wengi wakilia kukosa soko la maziwa, Chama cha Ushirika wa Utambuzi cha Busokelo, mkoani Mbeya wamesema uhakika wa kuuza lita 4500 za maziwa kila siku zimewafanya waongeze uzalishaji wa bidhaa hiyo.

 Akizungumza katika maonyesho ya Wakulima ya Nanenane, jijini Mbeya, Mwenyekiti wa chama hicho, Anyelwise Mwalukasa amesema awali hawakuwa na hamasa ya kufuga ng’ombe kama ilivyo sasa baada ya kuwa na uhakika wa soko.

Anyelwisye amesema maziwa yote wanayozalisha, wanauza kwenye kiwanda cha Asas cha Mjini Iringa.

“Tulipewa maarifa na baadae tukapata mtaji wa kutosha, hivi navyosema tumepokea ng’ombe kutoka Afrika Kusini, tunao uhakika wa kutajirika kutokana na ufugaji wa ng’ombe hawa,” amesema Mwalukasa.

Mfugaji wa ng’ombe kutoka chama hicho, Elly Mwaikenda alisema anao ng’ombe watatu wanaompatia zaidi ya lita 60 kila siku.

“Huyu ng’ombe unayemuona hapa nimempokea siku chache zilizopita toka Afrika Kusini, ameshazaa ndama na kwa siku ninakamua zaidi ya lita 17,” amesema.

Awali, Afisa Mifugo wa Afrifarm, Joshua Mwakasapi alisema inawezekana wafugaji wa ng’ombe kuvuna mamilioni ya fedha ikiwa watafuata misingi bora na kanuni za kazi hiyo.

“Huwezi kuwa na uhakika wa soko kama hufuati misingi bora ya ufugaji, inawezekana tu kama utakuwa muumini wa kanuni bora.