Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utitiri wa kodi wachosha wafanyabiashara

Muktasari:

Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mkutano wa elimu kwa mlipakodi kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2016/17 na mashine za kielektroniki (EFD) uliondaliwa na TRA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) na Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) mkoani Tanga.

Tanga. Wafanyabiashara jijini hapa, wameiomba Serikali kuondoa utitiri wa kodi zinazokusanywa na vitengo tofauti na kuunganisha kwenye tozo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mkutano wa elimu kwa mlipakodi kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2016/17 na mashine za kielektroniki (EFD) uliondaliwa na TRA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) na Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) mkoani Tanga.

Mbele ya mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa aliyemwakilisha mkuu wa mkoa, wafanyabiashara hao walisema utitiri wa ushuru na kodi unawapa usumbufu.

Mkurugenzi wa hoteli ya Macarious, Filbert Mmassy alisema amekuwa akitozwa kodi za aina 20 na kila moja ina kitengo chake kutoka halmashauri ya jiji, TRA na vyombo vingine ambavyo hufuatwa na wakusanyaji tofauti.