Uzalishaji umeme wa gesi asilia waongezeka

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tazania (TPDC), Mussa Mohamed Makame

Muktasari:

  • Kiwango cha uzalishaji wa gesi umeongezeka ambapo zaidi ya asilimia 85 inayozalishwa katika vitalu hivyo huenda katika uzalishaji wa umeme na kufanya mchango wa nishati hiyo kwenye grid ya Taifa kufikia asilimia 70.

Mtwara. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Mohamed Makame amesema kuwa viwango vya uzalishaji wa gesi katika visima vitano vya Mnazibay Msimbati umeongezeka ambapo zaidi ya asilimia 85 inayozalishwa katika vitalu hivyo huenda katika uzalishaji wa umeme nchini na kufanya wa mchango wa gesi asilia katika kuzalisha nishati hiyo kwenye grid ya Taifa kufikia asilimia 70.

Akizungumza wakati akikagua miundombinu ya gesi Mnazibay Msimbati amesema kuwa kwasasa kitalu cha Mnazibay gesi kinazalisha katika visima vitano ambavyo ni mnazibay namba 1-4 na msimbati namba 1 na kufanya hali ya uzalishaji kuwa nzuri.

“Kwa sasa hakuna tatizo lolote wala hakuna kisima kilichokauka katika vitalu vyote vya Mnazibay na Songosongo ambavyo vinachangia katika uzalishaji wa umeme nchini ambapo kwa leo zaidi ya megawati 850 zimeweka kutumika katika grid ya taifa,” amesema Makame.

Nae Meneja uzalishaji kutoka TPDC, Mhandisi Felix Nanguka amesema kuwa kitalu cha Mnazibay pekee kinazalisha futi za ujazo million 120 kwa siku ambapo ni mojawapo mwa kisima kinachozalisha gesi kwa wingi.

“Tunazalisha gesi kwaajili ya matumizi makubwa kama umeme huku tunakiwa na mikakati ya kuongeza tatifi zaidi na uzalishaji zaidi ili kuweza kukidhi mahitaji yanaoongezeka nchini.

Kitalu hiki awali kilikuwa kikizalisha futi za ujazo milioni 14 lakini juhudi zilifanywa na kuongeza uzalishaji na kuongeza futi za ujazo 6 mpaka 7 kwa siku na bado mipango madhubuti imewekwa ili kuweza kuongeza uzalishaji huo,” amesema Nanguka.