Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Bashungwa aiagiza Tanroads kurejesha mawasiliano Dar - Pwani

Muktasari:

  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewataka mameneja wa Tanroads kukagua madaraja katika maeneo yao ili kupata takwimu na hali halisi ya uharibifu unaofanywa na mvua.

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), kuhakikisha daraja la Mingoi linalounganisha mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo linakamilika haraka.

Picha za video zilizosambaa mitandaoni jioni ya leo Desemba 8, 2023 zimeonyesha wananchi wakishangaa shimo lililojitokeza juu ya daraja hilo.

Akizungumza kupitia video iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Waziri Bashungwa aliye katika ziara mkoani Shinyanga, ametoa pole kwa wananchi wanaotumia daraja hilo akisema linafanyiwa kazi.

"Nitoe pole kwa changamoto ambayo imejitokeza kwebye daraja linalounganisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, kwa maana barabara ya kutoka Tegeta kwenda Bagamoyo, tumepata changamoto ya mawasiliano.

"Nitumie nafasi kuwapa pole abiria ambao wanapata kadhia kwenye hili eneo. Lakini Wizara kupitia Tanroads timu imeshafika site kutathmini hali ya eneo," amesema.

Barabara ya Tegeta-Bagamoyo yafungwa kwa muda

Huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bashungwa amesema mameneja wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wameshafika hilo eneo na kutathmini hali ya daraja hilo.

"Ili kuwa na tahadhari, tumesitisha matumizi ya daraja hilo na tumetengeneza barabara kwenda Tamko Kibaha ili kuingia Dar es Salaam.

"Kwa taarifa za awali, kufika jioni mawasiliano yanarudi," amesema.

Pia amemwagiza Mtendaji mkuu Tanroads kuwaagiza mameneja wa mikoa wa Wakala huyo kuangalia hali ya madaraja nchini, wakati mvua zinaendelea kunyesha.

"Maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwetu Wizara ya Ujenzi ni kuhakikisha pamoja na changamoto za mvua za El-nino zinazoendelea, mawasiliano, iwe ni barabara ya changarawe iwe ni barabara ya lami yanaendelea kuwepo.

Ametoa wito kwa wananchi katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, wanaotumia vyombo vya moto kuchukua tahadhari.

"Wanaotumia mabasi ya abiria, malori na magari ya familia kwanza tuwe salama tukiwa barabarani, tupunguze spidi.

Amewataka Mtendaji Mkuu wa Tanroads na Mkurugemzi wa matengenezo waweke utaratibu wa kuhabarisha kuhusu hali ya barabara zote za changarawe na lami.

"Muunde group ambalo kila meneja atakuwepo. Na mimi mniweke, Katibu mkuu, Naibu Waziri wa ujenzi iki tuweze kujipanga kipindi hiki tunapoendelea na mvua za El - nino.