VIDEO: Dk Gwajima azungumzia kuenea kwa Corona Tanzania

Dk Gwajima azungumzia kuenea Corona Tanzania

Muktasari:

  • Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima amesema  Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo kila mtu avae barakoa kwenye mikusanyiko, hivyo watu wachukue tahadhari.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima amesema  Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo kila mtu avae barakoa kwenye mikusanyiko, hivyo watu wachukue tahadhari.

“Kasi ya wagonjwa kuendelea kujitokeza na kulazwa kwenye hospitali zetu inaashiria maambukizi yapo, watu wasidhani kwamba tunasubiri mpaka iwe mtaani tunaona maiti ndiyo tuanze kazi, kazi inayofanyika ni kuhakikisha hali haiwi mbaya.

“Serikali inajitahidi na Rais amekuwa akikumbusha jamani ndugu zangu tuchukue tahadhari na kujikinga na corona,” amesema Dk Gwajima.

Alitahadharisha kuwa kutokana na kinga ambazo Watanzania wanazo, wasiache kujikinga kwa kuwa wagonjwa wapo na wanaendelea kujitokeza.

“Tunaomba wale ambao hawaitikii tahadhari basi waitikie ili tuongeze wigo ili hali izidi kuwa salama zaidi tusipate idadi kubwa ya wagonjwa, kwenye msongamano vaa barakoa, inawezekana umepona huumwi umebeba unavisambaza, waokoe wengine, kuna wazee na wengine wanaumwa, tukivaa wengi hizi barakoa tunawaokoa wasiovaa,” amesema Waziri Gwajima.