VIDEO: Dk Mwinyi awaandikia barua ACT-Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Dk Mwinyi awaandikia barua ACT-Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Muktasari:

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema amekiandikia barua chama cha ACT- Wazalendo kukiomba kupeleka jina la makamu wa kwanza wa Rais baada ya chama kupata asilimia ya zaidi ya 10 kwa mujibu wa Katiba.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema amekiandikia barua chama cha ACT- Wazalendo kukiomba kupeleka jina la makamu wa kwanza wa Rais baada ya chama kupata asilimia ya zaidi ya 10 kwa mujibu wa Katiba.

Amesema hayo leo November 19, 2020 Ikulu Zanzibar alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari, alifafanua zaidi kuwa baada ya uchaguzi kwisha na chama hicho kupata zaidi ya asilimia 10, walifuata matakwa ya kikatiba ya kuwaandikia barua ili chama kipeleke jina la Makamu wa kwanza wa Rais lakini kwa kuwa jina hilo halijafika, wameiacha nafasi hiyo wazi.

Mwinyi ameeleza kuwa kwa mujibu wa katiba mgao wa nafasi za mawaziri kwenye baraza hilo  inategemea na uwiano wa idadi ya viti vya wawakilishi wa kuchaguliwa.

“Kwa maana hiyo chama cha ACT Wazalendo kina idadi ya viti vya uwakilishi waliochaguliwa, ndio maana nimeacha nafasi mbili endapo watakuwa tayari, lakini ukweli ni kwamba hadi leo hawajaenda kuapishwa kwa hiyo hawajasajiliwa kwa hiyo lazima tuwape muda wa kikatiba, hiyo ndio sababu,” amesema Rais Mwinyi.