VIDEO: Dk Mwinyi, Maalim Seif kuanza ziara ya siku mbili Chato

Thursday January 14 2021
By Rehema Matowo

Chato. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi na makamu wake wa kwanza, Maalim Seif Sharif Hamad leo asubuhi Alhamisi Januari 14, 2021 wataanza ziara ya siku mbili wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Akiwa Chato Dk  Mwinyi na ujumbe wake watakuwa na mazungumzo na mwenyeji wao, Rais John Magufuli.

Baada ya mazungumzo hayo Dk Mwinyi  na Maalim Seif watatembelea soko la kimataifa la dagaa la Kasenda na kuzungumza na wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo.

Dk Mwinyi ametua katika uwanja wa ndege wa Geita-Chato na kupokelewa na waziri wa Nishati,  Dk Merdad Kalemani na Waziri wa Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Maalim Seif aliwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kupokelewa na ujumbe wa viongozi wa Mkoa wa Geita.


Advertisement
Advertisement