Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO-Kilichomfanya mbunge akapiga magoti bungeni hiki hapa

Muktasari:

Vikao vya bunge la bajeti vinaendelea mjini Dodoma.


Dodoma. Mbunge wa Ileje (CCM) Janeth Mbene amepiga magoti bungeni na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kupeleka maendeleo kwenye wilaya yake anayodai ilisahaulika.

Mbene amefanya kitendo hicho leo bungeni Aprili 13, wakati akichangia bajeti ya ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Mara baada ya kuruhusiwa kuchangia bajeti hiyo, Mbene amesema wilaya ya Ileje ni ya miaka mingi lakini ilikuwa haina barabara ya lami lakini katika Serikali Awamu ya Tano, barabara imejengwa.

Katika kuonyesha kuwa jambo hilo limemfurahisha, mbunge huyo alipiga magoti, pembeni ya kiti anachoketi bungeni akimshukuru Rais Magufuli.