Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Magufuli amwagia sifa bosi TCAA, asema angekuwa na binti angemuozesha

Muktasari:

Rais wa Tanzania John Magufuli amemwagia sifa mkurugenzi mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri Anga Tanzania (TCCA), Hamza Johari kutokana na kufanikisha kwake mradi wa ufungaji wa rada katika viwanja viwili vya ndege nchini

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania John Magufuli amemwagia sifa mkurugenzi mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri Anga Tanzania (TCCA), Hamza Johari kutokana na kufanikisha kwake mradi wa ufungaji wa rada katika viwanja viwili vya ndege nchini.

Navyo ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINA) na Kilimanjaro (Kia). Songwe na Mwanza utekelezaji unaendelea.

“Safi sana hii ndio mifano ya vijana wanaojituma. Sina zawadi ya kukupa lakini mwaka huu (2019) ukiamua kwenda Hijja nitakulipia  ili ukamshukuru Mungu kwa utendaji wako,”

““Johari oyee. Kwa kweli wewe ni  Johari kweli  nasema kwa dhati bila unafiki nilifuatilia utendaji wake wa kazi yupo vizuri. Unamuona mtu anazungumza pointi ningekuwa na binti ningekupa ukaoa,” amesema Rais Magufuli.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika  hafla ya uzinduzi wa rada za kuongoza ndege katika uwanja  wa JNIA.

“Aprili 2019 tulikutana  hapa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa radi nne, leo tumekutana kwa ajili ya kuzindua radi iliyosimikwa hapa JNAI. Nimefurahi sana, wote mnajua mimi sipendi miradi inayoishia njiani hasa ninayoiwekea jiwe la msingi. baadaye unaambiwa haujakamilika,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli amewashukuru wabunge kwa kupitisha bajeti kwa ajili ya mchakato huo huku kuwataka waendelee kuchapa kazi.