VIDEO: Rais Kenyatta azungumzia kifo cha Rais Magufuli

Rais Kenyatta azungumzia kifo cha Rais Magufuli

Muktasari:

  • Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo Alhamisi Machi 18, 2021 ametoa salamu za pole wa wananchi wa Tanzania kufuatia kifo cha Rais, Dk John Magufuli kilichotokea jana katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Dar es Salaam. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo Alhamisi Machi 18, 2021 ametoa salamu za pole wa wananchi wa Tanzania kufuatia kifo cha Rais, Dk John Magufuli kilichotokea jana katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo Rais Kenyatta ameelezea uhusiano uliokuwepo kati yake na Rais Magufuli enzi za uhai wake huku akisema kuwa Tanzania imepoteza rafiki na kiongozi wa kweli aliyekuwa na lengo la kuunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Ninakumbuka mara nyingi tulikutana na kuongea kuhusu maendeleo ya nchi zetu mbili, safari yake rasmi alipotembelea Kenya tulifungua barabara na pia alinipatia heshima kubwa sana kwa kumtembelea mama yangu na pia alinialika Tanzania ambapo na mimi pia nilipata fursa ya kutembelea Chato na kuonana na mama yake na tulilala pale nyumbani kwake na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu uhusiano wetu kama wanachama wa Afrika Mashariki.

Rais Kenyatta ameahidi kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli nzima ya kuhakikisha kiongozi huyo anapumzishwa na kuendeleza uhusiano uliokuwepo kati ya Tanzania na Kenya.

“Asubuhi ya leo nilipata nafasi ya kungea na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kumpa pole na kumhakikishia kwamba tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania hadi kuhakikisha kwamba tumempuzisha rafiki yetu na kuendela na msimamo wake wa kuunganisha wananchi wa Afrika Mashariki,” amesema Rais Kenyatta.