VIDEO: Samia aelezea ugumu wa kiapo chake cha urais

#Live​: Samia Suluhu Hassan kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, historia mpya yaandikwa

Muktasari:

  • Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza hali aliyokuwa nayo wakati akila kiapo cha leo ni tofauti na viapo vingine alivyowahi kuvifanya siku za nyuma.

Dar es Salaam. Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza hali aliyokuwa nayo wakati akila kiapo cha leo ni tofauti na viapo vingine alivyowahi kuvifanya siku za nyuma.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema amekula kiapo akiwa na kidonda kikubwa moyoni mwake.

“Leo si siku nzuri kwangu ya kuhutubia taifa maana nimeelemewa na kidonda kikubwa kwenye moyo wangu. Kiapo nilichokula leo ni tofauti na viapo vyote nilivyowahi kuapa katika maisha yangu.

“Viapo vyote nilivyokula vilikuwa vya faraja, nderemo, vifijo na bashasha tele, leo nimekula kiapo cha juu zaidi kwenye nchi yetu nikiwa na majonzi tele na nchi ikiwa imetandwa wingi jeusi na simanzi kubwa,” aliongeza Samia.