VIDEO: Serikali yazungumzia miamala ambayo haikukatwa kodi

Serikali yaeleza mamilioni ambao hawajakatwa tozo ya miamala

Muktasari:

  •  Serikali ya Tanzania imesema watu milioni 30 wanaofanya miamala ya Sh1 hadi Sh999 kwa siku  hawakukatwa tozo ya kutuma na kutoa fedha.


Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema watu milioni 30 wanaofanya miamala ya Sh1 hadi Sh999 kwa siku  hawakukatwa tozo ya kutuma na kutoa fedha.

Hayo yamesemwa leo Septemba mosi,   2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba katika mkutano wake  na wanahabari akibainisha kuwa lengo ni  kuangalia ustawi wa jamii.

“Tumeachia miamala zaidi ya milioni 29 kwa watu ambao wanatumiana kuanzia shilingi moja mpaka Sh999, watu wanaotumiana viwango vile tuliiachilia yote ile kwa sababu dira ya rais sio kukusanya hela tu anaangalia na ustawi wa jamii,  amesema Nchemba.

Amesema kuwa tangu tozo ya miamala ya simu kuanza kutolewa wamekusanya zaidi ya Sh63 bilioni.

 “Ukiangalia tangu tuanze kukusanya hili suala hadi tarehe 30 yaani ujumla wake kwa mtililiko tunazaidi Sh63 bilioni,  hii nimejumlisha yote na ile ambayo tulishatoa iende kufanya kazi”