VIDEO: Siri ofisa aliyeuawa ofisini Dar

Wednesday October 13 2021
By Aurea Simtowe

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mbezi Msumi Wilayani Ubungo, Dar es Salaam, Kelvin Mowo akiwa ofisini kwake.

Kelvin aliuawa juzi saa 5:54 asubuhi alipokuwa akisikiliza mgogoro wa ardhi.

Mwananchi, lilifika katika ofisi yalikofanyika mauaji hayo na kukuta watu wakijadili namna unyama huo ulivyotekelezwa katika ofisi ya Serikali pasi na wahusika kuwa na hofu.

“Labda Mungu amependa aondoke kwa hali kama hiyo, lakini ni kwa ukatili sana….,” alisema Hamad Mawa ambaye ni mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi.

Akiwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kupigiwa simu baada ya tukio hilo, Mawa alisema alishtuka baada ya kuona ukatili aliofanyiwa Kelvin.

Alisema marehemu Kelvin alikuwa mtu wake wa karibu na mara zote aliomba ushauri katika mambo yaliyomtatiza wakati wa kutekeleza majukumu yake.

Advertisement

“Haya yote labda yasingetokea kama tungekuwa na kituo cha polisi, nasikitika kwa uchungu sana… alikuwa kijana anayeleta maendeleo kwa kasi mtu wa kushaurika wote walimpenda, sijui kama tutapata kijana mwingine kama huyu,” alisema Mawa.

Soma zaidi gazeti la Mwananchi leo Jumatano Agosti 13, 2021

Advertisement