Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Ummy Mwalimu aongoza mamia matembezi ya Ebola

Muktasari:

  • Matembezi ya hiari ya kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini ni maalum kwa ajili ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kuutambua ugonjwa huo, jinsi unavyoambukiza na namna ya kujikinga

Dar es Salaam. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo asubuhi Jumamosi Septemba 22, 2018 ameongeza mamia ya wananchi wa jijini Dar es Salaam katika matembezi ya hiari kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini.

Viongozi mbalimbali wameshiriki matembezi hayo wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari Kambi.

Matembezi hayo yameanza saa 1:00 asubuhi katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kupitia barabara ya Palm Beach na baadaye kuzunguka fukwe ya Coco Beach na kuhitimisha matembezi hayo katika ukumbi wa Karimjee saa 2:00 asubuhi.

Walioshiriki matembezi hayo walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka waliofariki katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere, kilichozama Septemba 20, 2018 katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.