Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video ya sheria za maadili yamuibua Waziri Gwajima, apaa kwenda kuwapongeza

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima akiwasikilizisha sauti na kuona video ya wanakijiji.

Muktasari:

  • Waziri amesema Sheria za maadili lazima zianzie ngazi ya familia na mabaraza ya wazee kwani zitasaidia kupunguza hata mauaji ya wazee.

Dodoma. Wakazi wa Kijiji cha Olevorusi Kata ya Kinyanki Arumeru wametajwa kuwa mfano wa kuigwa katika Maadili ya watoto.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jumanne Oktoba 3, 2023 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima wakati akizungumza na wazee wa Kata ya Hombolo.

Hivi karibuni ilisambaa mtandaoni video iliyowaonyesha wanakijiji hao wakipitisha Sheria kwa ajili ya kuwadhibiti vijana wanaokiuka maadili kijijini hapo.

Kwenye video hiyo, Mtendaji wa Kata alinukuliwa akiyataja mambo ya kuvaa nguo za kubana, kunyoa kiduku,uzururali na wanaume kuvaa heleni kuwa adhabu yake ni Sh50,000 au mhusika akishindwa anapaswa kufikishwa mbele ya wazee bila keleza anakwenda kufanya nini.

Leo Dk Gwajima amesema uamuzi wa wanakijiji hao ukimfurahisha na kuahidi lazima atafika kuwapongeza na kuwatia moyo katika kusimamia maadili ya vijana.

"Nawapongeza wanakijiji wale na ninaahidi kufika huko kuzungumza nao, naomba maeneo mengine nchini kite waige mfano huo mwema ambao nauona unakwenda kumaliza tatizo,"alisema Dk Gwajima huku akiwasikilizisha sauti ya video hiyo washiriki.

Waziri amesema Sheria za Vijijini na vikao kuanzia ngazi ya familia, koo na mabaraza ya wazee ndiyo suluhisho la kukomesha mauaji ya wazee nchini Tanzania.

Ameagiza vikao vya kuzungumza masuala ya kimaadili lazima vianzie ngazi ya chini kwenye familia kwani huko wanaweza kusikilizana na kusukuma ajenda mbele hata ngazi ya Serikali ambayo ina wajibu kusimamia watu wake.

Kiongozi huyo amesema baadhi ya watu wanaua wazee bila sababu wakati wanauaji wenyewe wanakuwa na msongo wa mawazo, tamaa ya mali na umasikini.

Hata hivyo taarifa ya Waziri inakuja zikiwa zimepita siku mbili baada ya taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Sindiga kutangaza vifo vya wazee wawili wa familia tofauti kwamba waliuawa na watoto wao, ambapo mmoja alihusishwa na tuhuma za kishirikina, wakati mwingine aliuawa kwa kosa la kumtambulisha mke mwingine akiwa na mtoto, kitendo kilichowakera.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Dodoma Mchungaji Petro Mpolo amesema maisha ya wazee wakati wote yamekuwa mashakani na mmomonyoko wa maadili kwa vijana haupimiki.

Mchungaji Mpolo ameomba Serikali iwasaidie kutunga sheria kali zenye adhabu kwa wapiga ramli chonganishi lakini akahimiza upande wa wazee kusomesha watoto ili kupunguza uzururaji.

Amewaasa wazee kusimama imara katika kupinga mila potofu kwa kusema wazi na kuripoti viashiria vya ukiukaji wa Maadili.