Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo wamzika Mrema Kiraracha

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP, Agustino Lyatonga Mrema likishushwa kaburini katika kijiji cha Kiraracha, Marangu mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali wameshiriki mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani nchini Tanzania, Agustine Lyatonga Mrema (77) nyumbani kwake, Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Moshi. Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani nchini Tanzania, Agustine Lyatonga Mrema (77) umezikwa leo Alhamisi Agosti 25, 2022 nyumbani kwao, Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro.

 Viongozi mbalimbali wa kisiasa na kiserikali wamehudhuria safari hiyo ya mwisho ya mwanasiasa huyo mkongwe nchini aliyefariki dunia asubuhi ya Jumapili ya Agosti 21, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Djinnis Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Utaribu amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.

Pia mawaziri wengine walikuwepo, Jumaa Aweso wa Maji na Hamad Masauni wa Mambo ya Ndani.

Aidha, mazishi hayo yumehudhuriwa na waziri mkuu mstaafu na makamu wa kwanza wa Rais, John Malecela.

Wengine ni wenyeviti wa vyama vya siasa, Freeman Mbowe wa Chadema, James Mbati wa NCCR-Mageuzi na Katibu wa  Chama Cha Mapinduzi-siasa na uhusiano wa kimataifa, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga.

Enzi za uhao wake, Mrema aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, naibu waziri mkuu, Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi anafikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Katika maziko hayo kila mmoja alimwelezea Mrema kama mtu ambaye anatazamwa kama baba wa siasa za mageuzi nchini kutokana na udhubutu wake wa kufanya siasa zilizoacha alama na zisizoumiza.