Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 350 Tanga kuwezeshwa kujiajiri, kuajiriwa

Muktasari:

  • Zaidi ya vijana 350 wa Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na mradi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa kupitia programu mbalimbali ikiwamo ya uchumi wa bluu.

Tanga. Zaidi ya vijana 350 wa Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika katika nyanja nne jumuishi za kuwapatia ujuzi na kujiajiri kupitia uchumi wa bluu chini ya programu ya vijana  ijulikanayo kama SASA.

Mradi huo utakaoendeshwa na Chuo Cha Ufundi Stadi (Veta) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga umetambulishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Mkuu wa Veta Tanga, Gideon Olerailumbe amesema mradi huu wa  utawagusa zaidi ya vijana 350 wakiwemo wanawake wa jiji la Tanga kwa asilimia 50.

Ametaja programu zilizopo chini ya mradi huo kuwa ni za kuwajengea uwezo wa kujiajiri au kuajirika vijana 150 ambao asilimia 50 ni wasio na ujuzi kabisa katika fani za usindikaji na uandaaji wa chakula, umeme wa jua, uchomeleaji na uungaji vyuma na utengenezaji wa mkaa mbadala.

Programu ya pili ni ya kuwapa ujuzi vijana walio sokoni ambao utagusa vijana 150 ikilenga asilimia 50 ya wanawake katika fani za usindikaji na uandaaji wa chakula, uvuvi, umeme wa Sola na uchomeleaji na uungaji vyuma wakati programu ya tatu ni ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo usio rasmi.

Amesema kupitia utekelezaji wa mradi huo Kwa kushirikiana na Shirika la ushirikiano wa kimataifa la Ubelgiji (ENABEL) kwa ufadhili wa umoja wa Ulaya pia kitaanzishwa kitengo cha utoaji wa ushauri wa masuala yanayohusu  ujuzi na huduma mbalimbali kwa wanafunzi.

"Lengo kuu la mradi huu ni kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi ili kuzalisha wahitimu wanahitajika katika soko la ajira na kuifanya Veta Tanga kuwa kituo cha umahiri wa utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwenye sekta husika, ili waweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kukamilisha mafunzo yao,"amesema Olerailumbe.

Mshauri mtaalamu wa ENABEL, Thomas Aikaruwa amesema Tanga ni miongoni mwa mikoa mitatu nchini Tanzania iliyomo kwenye  mradi huo ikiwamo Mwanza Pemba kusini na Kaskazini.

"Mradi wote unatazamia kugharimu Sh190 bilioni na unatazamiwa kumaliza muda wake mwaka 2027 ukifanya kazi na Veta, Sido, Halmashauri za miji na  Zanzibar,"amesema Akairuwa.

Balozi Batilda amewataka walio katika mradi huo kutumia vyema fedha pamoja na vifaa ili uweze kuleta tija kwa walengwa.

"Sina mashaka na utendaji kazi wa viongozi wa Veta lakini kama kuna jambo ambalo hatutaelewana ni usimamizi duni wa vifaa na fedha za mradi huu, mimi ni mfuatiliaji mzuri nitafuatilia kila kitu,"amesema Balozi Burian.