Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana wataja changamoto tano kilimo Afrika

Muktasari:

  • Kukosekana kwa taarifa sahihi, mitaji, ardhi, kuibuka kwa maradhi duniani kumetajwa na vijana kama changamoto zinazowakabili katika sekta ya kilimo.

Dar es Salaam. Kukosekana kwa taarifa sahihi, mitaji, ardhi, kuibuka kwa maradhi duniani kumetajwa na vijana kama changamoto zinazowakabili katika sekta ya kilimo.

Kufauatia changamoto hizo, Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka Serikali za Afrika kufanya mageuzi ya kilimo na sera katika nchi zao ili kuwawezesha vijana kuzalisha kuendana na mahitaji ya dunia.

Ametoa kauli hiyo katika mkutano wa wakuu wa nchi ndani ya Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF) linalofanyika jijini hapa.

Pia Rais Samia ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mchache tangu afanye mkutano na vijana wa Afrika na kuzungumzia kuhusu kilimo, fursa na changamoto wanazokutana nazo.

"Vijana walipata fursa ya kueleza changamoto wanazokutana nazo, ukosefu wa taarifa sahihi, mitaji, ardhi kuibuka kwa maradhi duniani na athari za mabadiliko ya hali ya hewa vinetajwa kuwa vikwazo," amesema Samia.

Amesema kuna fursa ya kufanya mageuzi ikiwa nchi za Afrika zitaangalia sera zake ili kuwawezesha vijana hao.

Amesema kwa upande wa Tanzania inafanya jitihada mbalimbali ili kuvutia wanawake na vijana katika kilimo ufugaji na uvuvi chini ya programu ya jenga kesho iliyobora (BBT) inayotekelezwa maendelo mbalimbali nchini.

"Pia tunafanya utekelezaji wa viwanda katika kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, kuimairhsa miundombinu ya umwagiliaji utafiti na mifumo ya mbegu bora na kuimarisha mifumo ya masoko," amesema Samia.