Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa dini Kilimanjaro wafurahia Mbowe kuachiwa

Muktasari:

  • Viongozi wa dini, Mkoani Kilimanjaro wameipongeza Mahakama pamoja na serikali kwa kumuachia huru kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe.


Moshi. Viongozi wa dini, Mkoani Kilimanjaro wameipongeza Mahakama pamoja na serikali kwa kumuachia huru kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe.

Viongozi hao wamesema kuachiwa  Mbowe kunafungua ukurasa mpya kwenye Taifa la Tanzania hususani kwenye suala la maridhiano na maelewano.

Wakizungumza na Mwananchi leo, Machi 4,2022 viongozi hao wamesema suala la kuachiliwa kwa Mbowe kunampa heshima kiongozi Mkuu wa nchi kwa uamuzi huo na kwamba jambo hilo lilikuwa likiwaumiza sana nafsi zao kama viongozi wa dini.

Akizungumzia kuachiliwa kwa Mbowe,Askofu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG) na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Kilimanjaro International Christian Centre(KICC),Askofu Glorious Shoo amesema kuachiwa kwa Mbowe kutaondoa uhasama na chuki ambazo zilikuwa zimejengeka kwenye baadhi ya mioyo ya watu

"Naipongeza serikali kwa kumuachia kiongozi huyu wa upinzani ni uamuzi ambao unafungua ukurasa mpya kwenye Taifa letu hasa kwenye maridhiano na maelewano,"

"Kila mtu anafurahia kusikia kiongozi huyu wa upinzani ameachiliwa na kwamba yuko huru kuendelea na shughuli zake,Jambo hili linampa heshima kiongozi Mkuu wa serikali kwa uamuzi huu uliosubiriwa kwa muda mrefu,"amesema Askofu Shooo

Naye Shekhe wa Mkoa huo,Shekhe Shaban Mlewa amesema suala la kushikiliwa kwa Mbowe lilikuwa likiwapa shida viongozi wa dini huku akiipongeza serikali kwa kuendelea kuwa sikivu kwa viongozi wa dini.

"Tunakipongeza chombo cha mahakama na serikali yetu kwa kuendelea kuwa sikivu na hatimaye kumuachilia huru kiongozi huyu wa upinzani maana viongozi wa dini tulikuwa tukipata shida kwenye nafsi zetu,"amesema Shekhe Mlewa