Vitali aachiwa, kuripoti polisi kesho

Msanii wa muziki, Vitali Maembe

Muktasari:

Hatimaye msanii Vitali Maembe aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani  Kibaha mkoani Pwani ameachiwa kwa dhamana.

Dar es Salaam. Hatimaye msanii Vitali Maembe aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani  Kibaha mkoani Pwani ameachiwa kwa dhamana.

Taarifa iliyotolewa kwa umma leo Jumatano Novemba 3, 2021 na Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalumu Taifa Chama cha ACT- Wazalendo, Mbarala Maharagande imesema kuwa Vitali ambaye pia ni mwanachama wa chama hicho ametakiwa kuripoti katika kituo cha polisi kesho asubuhi.

Maembe alikamatwa jana Bagamoyo na baadaye kuhamishiwa Kibaaha.

Awali katika taarifa ya Maharagande ilidai kuwa kuwa msanii huyo alikamatwa kwa tuhuma za kuwakashifu viongozi kupitia wimbo wake wa Kaizari.