Waangalizi wataka vijana, wanawake zaidi uchaguzi Kenya

Kiongozi wa wasimamizi wa Uchaguzi Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jakaya Kikwete amevishauri vyama vya siasa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya kuhusisha vijana na wanawake zaidi kwenye shughuli za uchaguzi.

Muktasari:

Kiongozi wa wasimamizi wa Uchaguzi Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jakaya Kikwete amevishauri vyama vya siasa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya kuhusisha vijana na wanawake kwenye shughuli za uchaguzi.

Nairobi. Kiongozi wa wasimamizi wa Uchaguzi Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jakaya Kikwete amevishauri vyama vya siasa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya kuhusisha vijana na wanawake kwenye shughuli za uchaguzi.

Kikwete ametoa ushauri huo leo Alhamisi Agosti 11, 2022 wakati akisoma ripoti ya awali ya hali ya uchaguzi nchini humo kwenye kituo kikuu ya kuhesabia kura cha Bomas ambapo amesema vijana wengi wamelalamika kutopewa nafasi za kugombea kwenye nafasi mbalimbali hivyo wameshauri wakati mwingine wahusishwe.

Kwa upande wa IEBC, Kikwete amesema kuwa misheni yao imegundua uhusishwaji wa wanawake na vijana kwenye usimamizi wa kura lakini jitihada za kuongeza idadi ya makundi hayo ziongezwe maradufu.

“Makamu wangu kwenye usiamizi yeye ni mwanamke na kwenye kila kituo tulichopita kuangalia amekuwa akiulizia juu ya idadi ya wasimamizi wanawake. Wasimamizi wa uchaguzi walikuwa na uelewa mkubwa na tunaishauri IEBC kutoa mafunzo na kuhusisha vijana na wanawake wengi kwenye usimamizi,”alisema.