Wabunge tisa watakaoiwakilisha Tanzania Eala hawa hapa…

Muktasari:

Bunge la Tanzania limewachagua wabunge tisa watakaoiwakilisha nchi hiyo katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala).

Dar es Salaam. Bunge la Tanzania limewachagua wabunge tisa watakaoiwakilisha nchi hiyo katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala).

Wabunge hao wamechaguliwa leo Alhamisi, Septemba 22, 2022 bungeni jijini Dodoma.

Kati ya wabunge hao tisa, mmoja ni wa upinzani kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye ni Mashaka Ngole.

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amewatangaza ni Angela Kizigha, Dk Shogo Mlozi, Nadra Mohammed, Dk Abdullah Makame, Machano Machano, Ansari Kachwamba, James Millya na Dk Ng'waru Maghembe ambao wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa wagombea walioangukia pua kwenye kinyang’anyiro hicho ni Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akizidiwa kura na Mashaka wote kutoka vyama vichache vyenye uwakilishi Bungeni kati ya