Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wa maendeleo waahidi Sh751.2 bilioni kwa ajili ya vijana

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Tanzania imepokea ahadi ya ufadhili wa zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh751.2 bilioni) kutoka kwa wadau wa maendeleo kwa ajili ya kuwasaidia vijana kwenye sekta ya kilimo.

Bashe amebainisha hayo leo Septemba 7, 2023 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo marais mbalimbali akiwemo William Ruto (Kenya), Macky Sall (Senegal) na Evariste Ndayishimiye (Burundi).

Amesema kama Tanzania, mwisho wa mkutano huo wameahidi fedha kwa ajili ya vijana na malengo yao yalikuwa ni kukusanya Sh2 bilioni kwa ajili ya vijana, hata hivyo wameahidiwa fedha nyingine kutoka kwa wadau.

“Benki ya Dunia imeahidi dola 100 milioni, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi dola 100 milioni, IFAD imeahidi dola 60 milioni, AGRA imeahidi dola 40 milioni na Bill and Melinda Gates Foundation pamoja na wadau wengine wameahidi kuanza mpango wa mabadiliko ya kilimo nchini Tanzania kwa miaka 25 ijayo.

“Kama Waziri wa Kilimo nawashukuru viongozi wote kwa kuonyesha uongozi wenu katika ukombozi wa pili wa bara la Afrika, kutengeneza ajira za staha kwa vijana, kuwezesha ufadhili kwenye kilimo, asanteni sana,” amesema Waziri Bashe.

Bashe ameeleza kwamba miaka michache ijayo, idadi ya watu ya Afrika itakuwa bilioni 2, ulimwengu utakuwa na watu bilioni 50.

“Tumeona dhamira yenu, tumeona shauku yenu ya kutaka kuibadilisha sekta ya kilimo kinachohitaji mabadiliko ulimwenguni na mifumo ya kimataifa ya fedha kupata usawa katika kugharamia mabadiliko hayo barani Afrika,” amesema waziri huyo.

Ameongeza kuwa leo wamekutana baada ya mkutano wa tabianchi uliofanyika Nairobi, Kenya na wanakutana kabla ya mkutano wa Cop28.

“Viongozi wetu mmetoa msimamo wa Afrika ambapo Afrika inataka usawa katika kufadhili masuala ya mazingira katika mabadiliko ya mifumo ya chakula na mawaziri wa kilimo tumekutana leo na mwisho wa mkutano huu tutatoa maazimio yetu yanayoakisi maazimio yalifofikiwa Nairobi na Dakar,” amesema.