Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wakosoa raia wa Afghanistan kurejeshwa makwao

Pakistan imezindua awamu mpya ya kampeni yake ya kuwarejesha makwao  maelfu ya raia wa Afghanistan hatua iliyokosolewa na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu.

Awamu hiyo mpya itawahusisha Waafghanistan walioishi Pakistan kwa miongo kadhaa, huku wengi wao wakiwa na vibali halali vya kuishi nchini humo.

Kwa mujibu wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Waafghanistan 800,000 wenye vibali vya kuishi Pakistan walitakiwa kuondoka nchini humo hadi kufikia  Machi 31 mwaka huu ambapo tangu kupita kwa tarehe hiyo, raia 8,906 wameondolewa kwa lazima nchini Pakistan.

Naibu mkurugenzi wa kanda ya shirika la Amnesty International, Isabelle Lassée alisema, ‘’uamuzi wa serikali ya Pakistan kuwaondoa wakimbizi wa Afghanistan si sahihi maana unakinzana na ahadi za awali za kudumisha haki za watu.’’

Kati ya Septemba 2023 na Februari 2025, mamlaka ya Pakistan iliripotiwa kuwafukuza zaidi ya raia 844,000 wa Afghanistan.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa serikali imeanzisha vituo 54 vya kuwahifadhi raia wa Afghanistan lakini kumekuwa na hali ya wasiwasi katika kambi hizo hasa kwa wanawake na watoto.

Abdul Motalib Haqqani, msemaji wa Wizara ya Uhamiaji alinukuriwa akilaani raia hao kurejeshwa makwao, akisisitiza kuwa ni kinyume na sheria na misingi ya dini.