Wafa kwa kula chakula chenye sumu

Muktasari:
Baada ya kula maandazi na kusikia maumivu ya tumbo, walipewa dawa za kienyeji za jamii ya wafugaji wa kimasai badala ya kupelekwa hospitalini.
Simanjiro.Watoto wawili wa familia moja kwenye kitongoji cha Nadosoito wilayani hapa wamefariki dunia na wengine wawili kunusurika baada ya kula maandazi yanayosadikiwa kuwa na sumu.
Baada ya kula maandazi na kusikia maumivu ya tumbo, walipewa dawa za kienyeji za jamii ya wafugaji wa kimasai badala ya kupelekwa hospitalini.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mahmoud Kambona amesema watoto hao walifariki Juni 14 saa 10:00 jioni na kuwataja waliofariki dunia kuwa ni Jonas Zebedayo (17) na John Zebedayo (14), huku Elizabeth Zebedayo (12) na Joshua Zebedayo (11) waliosurika wakiwa wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru wakitibiwa.
Amesema chanzo cha vifo vivyo ni chakula chenye sumu walichokula wakati wazazi wao hawapo nyumbani, lakini akasema wamechukua mabaki hayo na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili uchunguzi ufanyike kubaini chanzo.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz