Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahadhiri wa UDSM wakipeleka kitabu chao nchini Afrika Kusini

New Content Item (2)

Wanahistoria wawili wadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Maxilian Chuhila na James Zotto katika picha ya pamoja baada ya kukipeleka kitacho chao kuhusu Utengamano wa Africa, mgogoro wa Sahara nchini Afrika Kusini.

Muktasari:

  • Leo  Juni 11, 2024 wahadhiri hao wamefanikiwa kufikisha maudhui ya kitabu hicho katika Chuo Kikuu cha Johannesburg

Iringa.  Wahadhiri wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania, Dk Maximilian Chuhila na James Zotto wamefanikiwa kukipeleka kitabu chao kinachohusu Matarajio ya Utengamano wa Afrika; Mgogoro wa Sahara nchini Afrika Kusini.

Awali, Dk Chuhila na Zotto walifanya uzinduzi wa kitabu hicho kilichochapishwa na APE Network Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) mkoani Iringa na baadaye wakakipeleka Chuo Kikuu cha Kenyatta, nchini Kenya.

Leo  Juni 11, 2024 wahadhiri hao wamefanikiwa kufikisha maudhui ya kitabu hicho katika Chuo Kikuu cha Johannesburg huku wakipata nafasi ya kuzungumza na wanahistoria mbalimbali kutoka nchini humo wakiwamo wanafunzi na wahadhiri.

Dk Chuhila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Historia nchini, amesema kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu vilivyoonyesha kwa undani masuala ya utengamano wa Afrika hasa kuhusu mgogoro wa Sahara.

Kabla ya kuandika, wanahistoria hao wawili walifanya utafiti nchini Morocco kisha kuja na kitabu wanachoamini kama kikitumika vyuo vikuu kitaongeza uelewa kuhusu utenganao wa Afrika hasa mgogoro huo wa Sahara.

Akizungumzia hilo,  Zotto amesema utengamano wa Afrika ni silaha laini inayoweza kumaliza mzozo wa Sahara uliodumu kwa zaidi ya miongo miwili sasa.

Kwa upande wake, Dk Adeole Akiniya kutoka Chuo Kikuu cha Johannesburg amewapongeza wahadhiri hao kwa kukifikisha kitabu hicho Afrika Kusini.

Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Polisario wamekuwa wakilumbana kwa zaidi ya miongo miwili kuhusiana na udhibiti wa eneo hilo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa, Jimson Sanga amesema jitihada za wanahistoria hao zinapaswa kuigwa na wahadhiri wengine kwamba, badala ya kuandaa maudhui yanayoishia ndani ya nchi, wanaweza kusambaza duniani kote.

“Binafsi nimeona kumbe inawezekana, kama tunaweza kufanya tafiti za ndani ya nchi basi tunaweza kufanya tafiti nje na maandiko yetu yakatumika katika kutoa elimu vyuo vikuu mbalimbali,” amesema Sanga.

Amesema badala ya kuwa wanapokea maandiko na vitabu kutoka mataifa mengine, wanaweza pia kusambaza maudhuo hayo nje ya nchi.