Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wajanja ‘wajisevia’ ng’ombe wa Rais Samia mradi wa BBT

Muktasari:

Ng’ombe hao walitolewa kwenye kituo hicho kwa lengo la kunufaisha vijana kupitia mradi wa ‘’Jenga Kesho Iliyobora’’ maarufu kama (BBT).

Mwanza. Ni ujasiri wa kifisadi! Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa ujasiri waliokuwa nao watu wanaodaiwa kuiba ng’ombe sita kati ya 600 waliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kituo atamizi katika Ranchi ya Mabuki Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ng’ombe hao walitolewa kwenye kituo hicho kwa lengo la kunufaisha vijana kupitia mradi wa ‘’Jenga Kesho Iliyobora’’ maarufu kama (BBT).

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Oktoba 3, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Paulo Chacha amesema watu watatu tayari wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

‘’Ng’ombe wanne kati ya sita tayari wamepatikana na kurejeshwa na juhudi za kuwasaka wengine wawili waliosalia zinaendelea,’’ amesema Chacha

Amesema wizi huo umebainika baada ya Serikali kupata fununu za kutoweka kwa mifugo kwenye shamba hilo na kuweka mtego ukiwemo kufanya sensa ya mifugo na kubaini kuwa ng’ombe sita hawakuwepo zizini.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini uwepo wa mtandao wa wizi wa mifugo katika shamba la Mabuki na uchunguzi wa kina unaendelea kuubaini kabla ya kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Kituo atamizi kilichoko shamba la Mabuki kina vijana 60 wanaopata mafunzo atamizi ya ufugaji ambao ni sehemu ya wanufaika wa mradi BBT.

Meneja wa Chuo cha Ufugaji Kampasi ya Mabuki, Jackob Ngowi amesema licha ya changamoto zinazoibuka, wanafunzi 60 wanaopata mafunzo atamizi kupitia mradi wa BBT tayari wameanza kunufaika kwa kuweza kumudu kunenepesha na kuuza mifugo.

Pamoja na shughuli za ufugaji, vijana hao walioko katika mradi wa BBT pia hunolewa katika ujuzi na mbinu bora za kilimo na ufugaji wa samaki kwenye vizimba.