Wakala wa Misitu wakabidhi madawati 12,115

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe 

Muktasari:

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ramo Makani ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kukamilisha kutengeneza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya Novemba.

Mwanza. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umekabidhi madawati 12,115 mkoani hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ramo Makani ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kukamilisha kutengeneza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya Novemba.

Kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo bila kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100 ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na changamoto ya ucheleweshwaji wa utaratibu wa uvunaji mbao katika baadhi ya misitu.